Wednesday, February 7, 2018

MBUNGE RITTA KABATI AMETOA SH. 500,000 KWA UMOJA WA VIJANA WA KANISA LA KIKATORIKI KIHESA (UVIKAI)


Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza na vijana wa kanisa la kikatoriki parokia ya kihesa (UVIKAI) wakati wa kufunga kongamano la vijana hao
 Baadhi ya vijana wa kanisa la kikatoriki parokia ya Kihesa wakimsikiliza mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakatika wa kufnga kongamano hilo.

Na Fredy Mgunda,Iringa

UMOJA wa vijana wa kanisa la kikatoroki parokia ya Kihesa wamemwangukia mbunge wa viti maalum Ritta Kabati kuhusu ukosefu wa ajira ambao unaongeza umaskini katika kaya mbalimbali hapa nchini.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi mwenyekiti wa umoja wa vijana wa kanisa la kikatoriki kihesa (UVIKAI) Mussa Kihwele alisema kuwa vijana wengi kwa sasa hawana ajira za kudumu kutokana na kukoseka kwa nafasi za kazi hivyo kupelekea vijana wengi kuwa wadhurulaji.

“Mgeni rasmi ukipita mtaani utakutana na kilio kikubwa kwa vijana ni kukosekana kwa ajira na ndio maana kuna baadhi ya maeneo vibaka wengi wameongeza hasa pita maeneo ya stand yoyote ile utagundua hilo” alisema Kihwele

Kihwele aliongeza kuwa kukosekana na kwa miradi mingi ya kudumu nako kunachangia kukosekana kwa ajira hivyo tunaishauri serikali kuwa na miradi ya kudumu ili kuwa na ajira za kudumu ambazo zitapunguza ongezeko la vijana wa mitaani.

“Serikali ikiweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuna miradi mingi nay a kudumu utaona upungufu wa vijana mitaani hivyo tunaishauri serikali kufanya hivyo kwa kushirikiana na sekta binafsi ambazo zinanafasi kubwa katika maendeleo hapa nchini” alisema Kihwele

Aidha Kihwele alisema kukosekana kwa ajira kunasababisha kupunguza muamko wa vijana kushiriki katika makongamano mbalimbali ya kidini  kwa kukosa ada ya kulipia kushiriki kwenye kambi ambazo zinakuwa zimeandaliwa na umoja huo.

“Ndugu mgeni ukiangalia hapa unaona idadi imepungua ya vijana kushiriki katika makongamano ya makanisa hasa hapa tulipo mwaka jana kulikuwa na washiriki wengi tofauti na hali ilivyo hivi sasa yote hiyo ni kukosekana na ada ya ushiriki” alisema Kihwele

Lakini licha ya kuwa na changamoto hizo bado tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dr John Magufuli anafanya kazi kubwa kuhakikisha kuna kuwa na ongezeko la ajira kwa vijana na wananchi wengine na ndio maana saizi anawaajiri vijana wengi kwenye vitengo mbalimbali vya serikali.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika kongamano hilo mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa anawachangia shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya kubuni mradi wa kufanya maendeleo ya kudumu.

“Naanza kwa kuwachangia hiki kidogo kwa ajili ya kuwawezesha kubuni kitu cha kufanya ila mungu akinijalia nitaongeza kwa mungu na kuongeza ajira kwa wananchi na vijana ambao wanalalamika ukosefu wa ajira” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa atawasaidia kuwaletea wataalamu wa kufundisha ujasiliamali ambao utasaidia jamii kujiajiri na kuacha kutegemea ajira kutoka serikali au kwenye sekta binafsi.

“Haya mambo ya kutegemea kuajiriwa serikali inatakiwa watanzania tuondokane na kasumba hiyo hivyo ni lazima tujtengenezee mazingira ya kujiajiri kuliko kutegemea kuajiriwa na serikali” alisema Kabati

Lakini Kabati aliwataka vijana kujipendekeza kwa mungu kuliko kujipendekeza kwa watu ambao hawana faida katika maisha ya sasa.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More