Wednesday, March 23, 2016

Watumishi HEWA Anzeni Kujiondoa

Mkuu  mpya  wa  Mkoa  wa  Kagera,Meja  Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amewaagiza  watumishi  wasio  na  sifa za  kuajiriwa kujiondoa  kabla  ya March  31  mwaka  huu.

Kijuu  alitoa  kauli  hiyo  jana  wakati  wa  Makabidhiano  ya  ofisi baina  yake  na  mkuu  wa  mkoa  wa  zamani,John Mongella ambapo alisema  kwamba  Tanzania  inawatumishi  hewa  zaidi  ya 2000, hivyo ana imani  hata  Kagera  wapo.

"Hao watumishi  hewa  endapo  watang'ang'ania kubaki katika vitengo  walivyopo  nitawashughulikia wahusika  wakuu  wa  vitengo  hivyo," alisema

Aidha, aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa mabaraza  ya  usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi  mkoa  ili  kusimamia  haki  za  wananchi.

Pia  aliwataka  watumishi  wa  serikali  mkoani  humo kufahamu maudhui ya "Hapa Kazi Tu", kwa kufanya kazi kwa kasi,haraka, nguvu, maarifa  na  uadilifu.

Aliwataka  kutosubiri  kusukumwa, lakini wajitambue wao ni akina  nani na  wanapaswa  kufanya  nini  kutokana  na  majukumu  waliyopewa.

Alisema  ili  kufikia  lengo  la  Rais John Magufuli la kuwatumikia wananchi  kwa  uaminifu  ni  lazima  kushikiria  uadilifu  na  kutambua  kwamba watumishi wapo kwa ajili ya kutoa huduma kwa jami

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More