Tuesday, March 1, 2016

SOSOPI AWAONGOZA BAVICHA KUTOA MSAADA SHILINGI MILIONI MOJA NA LAKI MBILI KWA WAATHIRIKA WA TARAFA YA PAWAGA

 Mwenyekiti Bavicha Patrobas Katambi akimkabidhi moja ya vitu walivyotoa msaada akiwa sambamba na makamu mwenyekiti wa bavicha patrick ole sosopi kwa wahanga.

 mwenyekiti bavicha Patrobas Kitambi akizungumza na waathirika wa mafuriko walioko kambi ya Kasanga tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa mkoani Iriringa.


Waathirika wa mafuliko yaliyotokea katika tarafa ya pawaga mkoani iringa wamepewa msaada uliogharimu shilingi milioni moja na laki mbili na baraza la vijana la chama cha demokrasia na maendeleo taifa (BAVICHA).

Akizungumza wakati wa utaoaji wa zawadi hizo makamu mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA OLE SOSOPI amesema kuwa wataendeleo kuwasaidia kila mara wanapopata kutokana na waathirika kupoteza makazi na chakula na kuwaomba wapokee msaada walionao.

“Nilikuwa safarini lakini nilipata taarifa ya majanga yenu kupitia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii niliumia sana na ndio maana niliamua kufunga safari kuja hapa kuwajua hali na kutoa chochote nilichonacho”.alisema

Aidha sosopi alipa pole kwa waathirika wa mafuko na wale waliopata kipindupindu na wale waliopoteza katika kipindi hicho kigumu na kuwaomba wananchi na viongozi mbalimbali kuendlea kuwaombea waliopoteza maisha na waliothirika.

“Jamani tuondoe itikadi zetu za vyama,dini na kabili katika kipindi hiki kigumu ina paswa kuishi kwa upendo na umoja ili kutumia imani na amani tuliyonayo na kuacha kuwatenga walioathirika”.alisema sosopi

Lakini sosopi aliongoze kwa kusema kuwa nitaendelea kushirikiana na nyie kwa njia moja au nyingine ili mradi mrudi katika maisha yenu ya kawaida na kusahau kama ulimkumbwa na majanga.

Sosopi amewashukuru wananchi waliokuwa wamejitokeza kuwa kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kuwaambia kuwa yeye ni mbunge wa wananchi kwa kuwa walimpigia kura nyingi sana na kumfanya kuwa mshindi wa pili nyuma ya mbunge wa sasa wiliamu lukuvu

“Tupo hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa pole walioathirika na maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi katika hali tulivu baada ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema sosopi

Naye mwenyekiti wa waarithirika wa mafuriko hayo ABDULI NGILI amewashukuru viongozi wa BAVICHA na serikali kwa misaada wanayoipata na kuwaomba kuendelea kuwasaidia kwenye maeneo magumu yaliyoharibiwa wakati wa mafuriko.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya RICHARD KASESELA amesema kuwa serikali haijawatelekeza waathirika wa mafuriko hayo,serikali itaendelea kuwasaidia waathirika kwa kadri inavyowezakana.

Patrobas Kitambi ni mwenyekiti bavicha taifa ameitaka serikali kutoa misaada kwa kufikili sio kwa kukurupuka kwa kutoa misaada ya aina moja tu wanapaswa kufanya uatafiti wa nini wananchi wanahitaji na sio kupeleka misaada tu.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More