Wednesday, March 30, 2016

IRFA YAUNDA KAMATI ITAKAYO SIMAMIA CHAGUZI MBALIMBALI MKOA WA IRINGA

 
 Ramadhani Mahano
NA RAYMOND MINJA IRINGA.
CHAMA cha mpira wa miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) kimetauwa  kamati ya uchaguzi itakayosimamia chaguzi mbalimbali mkoani Iringa.


Uteuzi wa kamati hiyo unaelezwa kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza migogoro iliyoko ndani ya vilabu pindi wanachama wake wanapotaka kuitisha uchaguzi lakini kunatokea migongano kati ya wanachama na viongozi wao .

Akizungumza na Bibwa  ofisini kwake Kaimu Katibu Mkuu wa IRFA,Ramadhani Mahano alisema kuwa walifikia maamuzi hayo  ya kuunda kamati  hiyo katika kikao cha wadau kilichoitishwa na mwenyekiti wake Cypriyan Kuyava kilichofanyika juzi ili kumaliza migogangano ndani ya vilabu  .

Mahano alisema kamati hiyo itaongozwa na mwenyekiti wake  ambaye ni Gaster Mdegela na makamu mwenyekiti akiwa ni Jakson Chaula .

Alisema kuwa kamati hiyo pia itakuwa na wajumbe sita ambao ni Lupyana Masawa ,Willy Chikweo,Shemu Mhen pamoja na Happness Nduguru

Hata hivyo Mahano alibaimisha kuwa kamati hiyo pia itangozwa na wanasheria wawili na wajumbe wake ni wanafamilia na wapenzi wa soka na kamati hiyo itaanza kazi mara moja baada ya uteuzi wake .

Alisema licha ya kuunda kamati hiyo ya uchaguzi hapo awali  chama chake kililazimika kuunda kamati sita ikiwemo kamati ya Ligi na Mashindano ambayo mwenyekiti wake atakuwa David Mwamalekela makamu atakuwa Pascal Bella ambapo wajumbe watakuwa Carlo Mbinda, Gutram Kawonga, Cletus Kifyoga, Nikolina Sanga, July Sawani na Isiaka Majaliwa.

Mahano alisema kuwa Kamati ya Waamuzi itaongozwa na David Lugenge akiawa na wajumbe Julias Mkomwa, Mwanaheri Kalolo, Abuu Yunus na Atilio Mnyeke.

Alisema kwa upande wa Kamati ya Mipango na Uchumi mwenyekiti atakuwa Stanford Mwakasala na wajumbe wa kamati hiyo watakuwa Abdallah Kiyumbo, William Kessy, David Wapalila, Jonnie Nkoma, Daniel Kindole, Rukia Muwango, Musa Kamtande na Victor Chakudika.


Alisema kuwa Kamati ya Maendeleo wanawake na  Vijana, Mwenyekiti wake ni Maulidy Toffy, huku wajumbe wakiwa ni Coster Magolosa, Tigana Lukinja,Gift Mwachang’a,Edina Ndelwa,Thadeo Lukosina Haruna Mduda.

Mahano aliongeza kuwa kamati ya Nidhamu na Usuluhishi mwenyekiti atakuwa ni Ignas Seboa Lutalemwa akifanya kazi na wajumbe Stanslaus Matutu, Devotha Chaula na Fredrick Amando.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More