Thursday, March 24, 2016

Hukumu ya Kutoa Lugha Chafu Inayomkabili Mbunge Saed Kubenea Itatolewa April 13

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda inayomkabili Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, Aprili 13, mwaka huu.

Hukumu hiyo itatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka unaowakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa na upande wa utetezi ukiongozwa na Peter Kibatara kuwasilisha hoja zao za mwisho.

Uamuzi huo ulitolewa jana na mahakama hiyo baada ya Kubenea na mashahidi wake watatu, akiwamo mwandishi wa New Habari 2006, Shabani Matutu na Josephat Isango wa Mwanahalisi kutoa ushahidi wao.

Akitoa ushahidi wake, Matutu alidai kuwa Desemba 14, 2016 katika Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd kilichopo Mabibo External kwenye mgomo wa wafanyakazi, hakusikia Kubenea akimuambia Makonda kuwa ni mjinga, mpumbavu, kibaka na cheo chenyewe kapewa.

Alidai alimsikia mbunge huyo akimuuliza Makonda “kwa nini unafunga mkutano bila ya kunipa nafasi ya kuongea wakati mgogoro nimeuanza mimi kuutatua, mimi siyo kibaka nimekuja baada ya kuitwa na wananchi walionichagua kwa kura 87,000”.

Kubenea anadaiwa kumtolea lugha chafu Makonda alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More