Friday, March 31, 2017

UZALISHAI wa mbegu bora za mazao mbalimbali ya kilimo nchini bado ni changamoto

NA MZIDALAFA ZAID(ARUSHA)
UZALISHAI wa mbegu bora za mazao mbalimbali ya kilimo nchini bado ni
changamoto kubwa kutokana na mbegu bora zinazozalishwa kutokukidhi mahitaji
ya soko linalotokana na ongezeko la wakulima wanaotumia mbegu hizo kwenye kilimo. 
Hayo yameelezwa leo na Meneja wa Shamba la mbegu la serikali, ASA,la mkoa
wa Arusha, Zadiel Mrinji, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa baraza la
wafanyakazi ambao ni wataalamu wa uzalishaji wa mbegu bora kutoka mashamba
yote tisa ya serikali yaliyopo kwenye kanda saba nchini,waliotembelea
shamba la mbegu bora la serikali la mkoa wa Arusha ,lililopo Ngaramtoni
wilayani Arumeru.
Mrinji amesema licha ya kuwepo wazalishaji wa mbegu bora kutoka nje
uzalishaji mbegu bora za kilimo ni asilimia 70% tu hivyo hazitoshelezi
mahitaji.
Mrinji , amesema shamba la mkoa wa Arusha ambalo lina ukubwa wa hekta 576 linazalisha asilimia 50% ya mbegu bora ambazo zilizofanyiwa utafiti wa wa
mazao ya Mahindi, Mbaazi, Maharage, alazeti,Ngano.
Mbegu hizo ambazo zimefanyiwa utafiti zina sifa ya kuvumilia ukame ambapo
wakulima hupata mazao mengi kutokana na kutumia mbegu hizo ambazo huzaa sana na hazishambuliwi na magonjwa .
Amesema ili wakulima waweze kupata mazao mengi zaidi ni kuwa karibu zaidi
na wataalamu wa ugani waliopo kwenye maeneo yao ambao watawapatia ushauri
wa kitaalamu namna ya kutumia mbegu bora za mazao yao wanayolima Kwa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti.
Mrinji,amesema kuwa shamba hilo likishazalisha mbegu bora za mazao
mbalimbali huwauzia mawakala wa pembejeo ambao huwauzia wakulima ambao hupatiwa ushauri wa kiteknolojia kutoka kwa maafisa ugani waliopo namna ya kutumia teknolojia katika kilimo .
Amesema changamoto iliyopo ni mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa yakiathiri uzalishaji wa mazao hali hiyo ililazimu shamba hilo
lililoaanzishwa mwaka 2006 kulazimika kuzalisha mbegu bora zinazovumilia ukame.
Kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mbegu feki, Mrinji amesema tayari serikali ilishaanzisha kitengomaalumu cha kudhibiti mbegu feki.
Amesema lengo ni kumuwezesha mkulima kutumia mbegu bora kuzalisha mazao mengi kwa kuwa mbegu hizo zinazozaa sana , zinavumilia ukame na wala hazishambuliwi na magnjwa,.
Akifungua kikao cha baraza hilo, kilichofanyika ukumbi wa kituo cha kulelea Yatima cha SOS,kilichopo Ngaramtoni , mkurugenzi wa masoko na mashamba ya mbegu bora nchini, ASA, Philemon Kawamala, amesema ASA ina majukumu manne ambayo ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mbegu bora ,kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kwenye uzalishaji wa mbegu bora .
Jukumu lingine ni kuhamasisha na kuelimisha wakulima kuongeza matumizi ya mbegu bora za mazao ,kushirikiana na watafiti waliopo kwenye kanda zote saba kwa ajili ya kuzalisha mbegu bora zinazotosheleza mahitaji .
Akawataka wajumbe wa baraza hilo kutambua kuwa wana jukumu kubwa la
kuhakikisha malengo ya uzalishaji mbegu bora za mazao unafikiwa ili kumuinua mkulima kutokana na kuzalisha mazao kwa kutumia mbegu bora.
Kwa upende wake msaidi wa shamba la Arusha, ambaye pia afisa killimo Marko
Mwendo, amewashauri wakulima kuwa kutunza risti pindi wanunuapo mbegu
kutokakwa mawakala lengo ni kuwezesha kufuatilia iwapo kutakuwepo na dosari kwenye mbegu hizo.
Amesema bila kuwa na risti itakuwa ni vigumu kuwezesha kutambua ni mbegu
zipi zenye matatizo ambazo zimesababisha kukosa mavuno waliyokuwa wameyatarajia

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More