Friday, March 31, 2017

DC SINGIDA AWEKA ZUIO KWA WANACHI KUTOKA NCHI ZA NJE KUINGIA MASHAMBANI KWA WAKULIMA NA KUNUNUA MAZAO


Na MZIDALFA ZAID,Arusha

serikali Wilayani Singida imepiga marufuku wafanyabiashara wa vitunguu
kutoka nchi jirani za Kenya,Uganda,Ruanda,Burundi,Zambia, Kongo na Malawi
kwenda kununu vitunguu kweneye mashamba ya wakulima vijijini na badala yake
amewataka kwenda kununua kwenye soko la kimataifa la vitunguu,lililopo
Manispaa ya Singida.
zuio lilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Singida,Bwana Eliasi Tarimo baada ya
kupokea malalamiko ya wafanyabiashara kutoka soko la kimataifa la vitunguu,
kulalamikia kuwa wafanyabiashara wanaotoka nchi hizo kuwa wanakwenda
kununua vitunguu kwenye mashamba ya vijijini na hivyo kusababisha biashara
katika soko hilo kudorora huku serikali ikikosa mapato yake.
Hata hivyo Bwana Tarimo hakusita kuwaeleza umuhimu wa tangazo hilo kuwa ni
kuhakikisha mkulima,mfanyabiashara wa kati na mfanyabaishara mkubwa kila
mmoja ananufaika na shughuli yake anayoifanya na kuwataka baada ya
kufanyabiashara zao wasisite kwenda kulipa kodi ili serikali iweze
kuwaletea maendeleo kwenye maeneo yao.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wa vitunguu katika soko hilo la
kimataifa,Bwana Jonathani Mpinga amesema kuwa serikali haina budi kuweka
usawa wa sheria ya kuzuia ujazaji kwa njia ya lumbesa kwa mikoa yote badala
ya sheria hiyo kutumika katika Mkoa wa Singida peke yake.
Mkuu huyo wa wilaya ameweka bayana kwamba akiwa mfanyabiashara wa zao hilo
amekwenda katika masoko ya Moshi na Mang’ola hajawahi kuona sheria ya
kukataza ujazo wa lumbesa kama inavyokatazwa katika Mkoa wa Singida na
hivyo kuishauri serikali kuwa na kauli moja kwa nchi nzima ili wanunuzi
wasije wakawakimbia katika soko hilo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More