Tuesday, March 28, 2017

MSOFE AWAOMBA KURA WABUNGE WA CCM

Na Fredy Mgunda,Iringa

Mfanyabiasha na Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji  wa mabsi ya Otta high classic Jeremia Msofe anaomba kura kutoka kwa wabunge wa chama cha mapinduzi (CCM) ili kupata nafsi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa bunge la afrika mashariki kwa kuiwakirisha Tanzania.

Akizungumza kwa njia ya simu Msofe alisema kuwa atahakisha lugha ya kiswahili inatumika barani afrika kama lugha mama kwa kuwa ndio lugha ilisamba zaidi barani afrika.

“Nimetembea nchi nyingi hapa afrika nimekutana na watu wengi wanazungumza Kiswahili hivyo hoja yangu itakuwa kuahakikisha natimiza kitu alichotuachia hayati baba wa taifa mwalimu Julias Kabarage Nyerere”.alisema Msofe

Msofe alisema kuwa atalazimaka kuwatetea wakulima kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania wengi ni wakulima na uchumi wetu bado unategemea kilimo hivyo ni lazima kuwekeza nguvu kwenye kilimo chenye tija na kufanikiwa kuinua mazao yanayozalishwa hapa nchi na kukuza uchumi.

“Tanzania tumebatika kuwa na ardhi nzuri na kubwa ambayo kwa asilimia kubwa bado haijatumika kwa mjibu wa wataalam wa kilimo hivyo ni lazima kutafuta nja mbadala ya kuwainua wakulima hawa ili kuviwezesha viwanda vyetu kupata mali ghafi nyingi na za kutosha ili kuinua kipato cha kila sekta hapa nchi”.alisema Msofe

Aidha Msofe amewataka watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi anazozifanya kwa kutafuta njia bora ya kuinua uchumi wa wananchi wake kutoka hapaulipo hadi kufikia uchumi wa viwanda kama sera yake alivyoielekeza kwenye Tanzania ya viwanda.

“Angalia sasa tunapata wawekezaji wengi kwenye sekta ya viwanda hii ni dalili nzuri ya kuukalibia uchumi wa viwanda hivyo nikiwa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki nitandelea kuunga mkono Rais kwa kutafuta njia za kuwanua wawekezaji wazawa ili waboreshe na kuanzisha viwanda vyao”.alisema msofe

Msofe aliwaomba watanzania kwa ujumla kumuombea ashinde kiti hicho ili aweze kuiwakirisha vyema nchi kwa uadilifu uliotukuka

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More