Wednesday, March 29, 2017

COSATO CHUMI ASAIDIA KUPATIKANA KWA TSH 230M KWA AJILI YA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI KATIKA HOSPITAL YA MJI WA MAFINGA

Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Bi Saada Mwaruka, Mhe Balozi Yoshida, Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi, mstari wa nyuma kutoka kushoto Mhandisi wa Halmashauri Venant Komba, Mganga Mkuu Dr Inocent Mhagama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mhe Charles Makoga na maafisa wa Ubalozi wa Japan Mara baada ya kusaini Mkataba wa Msaada wa Tsh 220m kwa ajili ya ujenzi wa Chumba cha Upasuaji kwenye Hospitali ya Mafinga
Mbunge Cosato Chumi akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Ubalozi Dr Tanaka mara baada ya hafla hiyo
Balozi wa Japan Masaharu Yoshida akizungumza wakati wa Hafla ya kusaini mkataba wa msaada wa tsh 220m kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji katika hospital ya Mafinga kufuatia maombi yaliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi  kwa Balozi mapema mwaka Jana
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi akitoa neno la shukran mara baada ya kusainiwa kwa mkataba wa msaada wa Tsh 220m kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji kwenye Hospital ya Mafinga zilizotolewa na Ubalozi wa Japan hapa nchini. Hafla hiyovya leo tarehe 29 March, 2017  ilifanyika kwenye makazi ya Balozi.


Ubalozi wa Japan Leo tarehe 29 March, 2017 umesaini mkataba wa usd 104,135 Sawa na Tsh 230m na Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Upasuaji kwenye Hospital ya Mafinga.

Akizungumza wakati wa kusaini kwa mkataba wa msaada huo, Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida alisema kwamba msaada huo ni matokeo ya Ombi la Mhe Cosato Chumi Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini aliloliwasilisha Ubalozini mwaka uliopita.

Aidha Mhe Balozi Yoshida alimpongeza Mbunge huyo kwa ushirikiano alioutoa hasa katika kufuatilia katika ngazi mbalimbali za serikali ikiwemo Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupata ridhaa ya kusaini mkataba wa msaada huo.

Pamoja na msaada huo, Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake hapa nchini, umetoa msaada kwa Halmashauri za Bukoba, Temeke na Chuo cha Ufundi Yombo.

Halmashauri ya Bukoba imepewa msaada wa usd 108,025 (Tsh (238m) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kwenye shule za Msingi za Nyakato na Kashozi ambazo ziliathiriwa na tetemeko la ardhi.
Kwa upande wa Temeke wamepokea msaada wa usd 137,837 (Tsh 274m) kwa ajili ya kuboresha Jengo la Huduma ya dharura kwenye Hospital ya Rufaa ya Temeke.
Chuo Ufundi Yombo wamepokea msaada wa usd 64,499(Tsh 130m) kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi wenye ulemavu.

Jumla ya usd 408,496 (Tsh 900m) zimetolewa katika misaada hiyo inayolenga kuwasaidia wananchi ngazi za chini yaani Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects .

Akizungumza Mara baada ya kusainiwa kwa mikataba ya misaada hiyo, Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi, alimshukuru Balozi Yoshida na Serikali ya Japan kwa kuendelea kufadhili miradi hasa inayolenga kuwafikia watu wa chini.

Aidha Chumi alimshukuru Wizara ya Fedha kwa kuridhia kusainiwa kwa mikataba ya misaada hiyo kabla ya kumalizika kwa mwaka wa Fedha wa Japan March 31. 'Namshukuru Sana Mhe Dr Philip Mpango na watendaji wake kwa jinsi ambavyo walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa taratibu zote za kisheria na kikanuni zinatimizwa kwa wakati ili mikataba hii iweze kusainiwa siku ya leo'

'Pamoja na misaada mikubwa kupitia ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yaani bilateral cooperation , bado Japan imeendelea kutoa na kufadhili miradi inayotekelezwa katika ngazi za chini kabisa, hili ni jambo jema na tunaopokea Fedha hizi tuzitumie kwa malengo yaliyokusudiwa' Alisema Chumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Bi Saada Mwaruka alisema kuwa msaada huo ni ukombozi kwa watu wa Mafinga na Mufindi kwa ujumla kutokana na ukweli kwamba Hospital hiyo inahudumia Wilaya ya Mufindi na hata Wilaya za jirani kama Mbalari na Iringa Vijijini.

Katika kipindi cha miaka mitano kuanzia kuanzia mwaka 2011 jumla ya usd 6.7m (Tsh 15bilioni) zimetolewa na Serikali ya Japan maalum kwa ajili ya kufadhili jumla ya miradi sitini (60) ya Afya, Elimu na Maji. Miradi hiyo imetekelezwa katika ngazi za Halmashauri.

2 comments:

Unknown said...

Safi sana...ila karibu kuweka habari kama heading ilivosema usichanganye na picha...umewataja watu wote wa kwenye picha inakujazia content bure...keep t up homie...t's me xric

Unknown said...

Safi sana...ila karibu kuweka habari kama heading ilivosema usichanganye na picha...umewataja watu wote wa kwenye picha inakujazia content bure...keep t up homie...t's me xric

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More