Wednesday, March 29, 2017

HIVI NANI WAKUTATUA MGOGORO WA TIMU YA LIPULI?

 hilo bango lina maneno ambayo tulikuwa tunaamini kuwa uongozi wa lipuli na wanachama wote wanapenda mpira na sio majungu lakini kinachoendelea saizi ndani ya club ya lipuli tofauti na hilo bago
Wadau wa soka mkaoni iringa bado wapo njia panda juu ya maandalizi ya timu ya lipuli kutokana na mgogoro uliopo baina ya kamati tendaji ya timu hiyo na Abu Changawe Majeki aliyefunguliwa na chama cha soka mkoa wa iringa.

Wakizungumza na blog hii wadau hao walisema kuwa  timu ya lipuli inahalibiwa na viongozi wachache walevi wa madaraka na pesa ambazo zitapatikana kutokana na lipuli kupanda hadi ligi kuu.

Msomali ni mmoja wa wajumbe wa kamati tendaji ya lipuli ambaye alisema kuwa ukitaka kuwa kiongozi ndani ya timu ya lipuli ni lazima upatane na Abuu Majeki au willy Chikweo hapo utakula kiulaini ila usipopatana na hawa viongozi basi wewe utageuka kuwa adui namba moja.

“Mimi ndio nahusika kutoa pesa bank za lipuli ila kiukweli Majeki na Chikweo ni waroho wa madaraka hasa linapokuja swala la pesa,hatuwezi kuendesha timu tukiwa na viongozi hawa wawili ni wanafiki na wanauchu wa madaraka mimi sipendi hivyo napenda mpira wa miguu uchezwe hapa nyumbani(Iringa)”alisema Msomali

Kwanini sasa wadau wanawalaumu na kuwatupia lawama viongozi hawa wawili Abu Changawe Majeki na Wille Chikweo?

 Abu Changawe Majeki alisema kuwa lipuli ni timu ya wanachama hivyo ni lazima tufanye uchaguzi ili tupate viogozi wenye uwezo wa kuendesha timu ya ligi kuu na sio kubaki na viongozi wasio na sifa ya kuendesha timu ya ligi kuu.

“Mimi binafsi nimerudi kuja kusimamia uchaguzi ili tupate viongozi wenye uwezo wa kuongoza timu ya ligi kuu lakini bila kujua nini tatizo najikuta nimefungiwa na wanaojiita kamati tendaji wakati kama hiyo hawana mamlaka ya kunifungia” alisema Majeki

Majeki  alisema kuwa viongozi wa lipuli wengi hawataki tuwe na wanachama wapya ndio maana hata kadi wamezificha majumbani kwao sasa hiyo ni aibu kubwa,kwanini hawataki tuwe na wanachama wapya.

“Haiwezekani timu ikawa na wanachama walewale kila siku ni lazima tufanye jitihada za kuongeza wanachama lakini kwanini wakina Chikweo na kundi lake hawataki na wanaweka masharti magumu kupata wanachama wapya na kwanini hawataki kunitambua kuwa mimi kiongozi wao wakati adhabu yangu imeisha?” alisema Majeki

Naye katibu mkuu wa timu ya lipuli Wile Chikweo alisema kuwa wamemfungia Majeki kutokana na kuvunja katiba ya timu ya lipuli kwa kuwapiga baadhi ya viongozi,wajumbe na wanachama wa timu ya lipuli.

“Mimi nishapigwa na majeki na ameshapiga viongozi wengine na kuna baadhi ya wananchama walishampeleka mahakamani kutokana na ubabe wake hivyo hapaswi kuwa kiongozi wa lipuli hata siku moja”alisema chikweo

“Wakati Majeki kafungiwa kulikuwa kumetulia na ndio maana tulifanikiwa kupandisha timu lakini hatujui njia gani ilimasawa kumfungulia Majeki wakati akiwa kwenye adhabu yake alikiuka mambo mengi ya adhabu hiyo mfano alijihusisha na mashindano ya msofe Cup” alisema Chikweo

Kuna mdau mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe hapa alisema kwanini chama cha mpira manispaa kimekaa kimya na kwanini chama cha mpira kimekaa kimya,basi ujue kuwa Chikweo bado anafitna na baadhi ya viongozi kutokana na uchaguzi uliopita na ndio maana kuna makundi mawili, kundi moja linamsaidia majeki na kundi lingine lipo pamoja na kamati tendaji ya lipuli na ndio linalotoa maagizo yote hivyo naomba viongozi wa wilaya kam mkuu wa wilaya Richard Kasesela na Mkuu wa mkoa Bi Amina Masenza kuingilia kati mgogogoro huo.

Hivi ni kweli malkia wa lipuli madam Jesca msambatavangu,mwemyekiti wa mipango na fedha wa lipuli jully sawani,katibu wa lipuli fc lonjino malambo, katibu wa IRFA ally ngalla,Mjumbe wa mkutano mkuu TFF abuu silia, Mwemyekiti wa Chama cha Soka Manispaa ya iringa lupyana masawa, mwakilishi wa vilabu manispaa Michael Mlowe na mjumbe wa kamati tendaji IRFA david wapalila mnashindwa kuwaita Majeki na Chikweo mkazungumza nao ili kumaliza mgogoro huu.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More