Monday, March 27, 2017

LIPULI BADO PANAFUKA MOSHI

Abu Changawe Majeki akiongea na waandishi wa habari wa Mkoani iringa juu ya sakata lake la kusimamishwa uenyekiti wa timu ya lipuli
Baadhi ya wadau wa lipuli na waandishi wa habari wakimsikiliza Abu Changawe Majeki
Hawa ni baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya timu ya lipuli walijibia tuhuma silizotolewa na Abu Changawe Majeki

Na Fredy Mgunda,Iringa

Kamati tendaji ya time ya mpira ya lipuli imesema kuwa bado haimutambui aliyekuwa Mwenyekiti wa timu hiyo kutokana na kuendelea kukiuka kanuni na Katiba ya timu hiyo

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari  viongozi wa kamati ya timu ya lipuli wakiongozwa na Wille Chikweo na Lonjino Malambo walisema kuwa Abuu Changawe majeki kukaa kimya na kuacha kuongea na vyombo vya habari.

Longino alisema kuwa kamati ya utendaji ina uwezo wakumsimamisha kiongozi yeyote iwapo ataonekana kuwa mwenendo wake uko tofauti na Katiba ya timu ya lipuli atachukuliwa hatua bila kuwa na huruma.

"Timu sasa inaonekana inamigogoro kutokana na mtu mmoja hatuwezi kuendeshwa na Majeki kwa matakwa yake wakati lipuli inakatiba yake inayoifanya ijiongoze na sio kuongozwa na mtu kwa kuvunja Katiba".alisema Lonjino

Aidha lonjino alisema kuwa Majeki hajawahi kuwa mwanachama hai kwa sababu hajalipa ada ya uwanachama wake kwa muda mrefu hivyo inatosha Kabisa kumsimamisha kwakuwa sio kiongozi wa kuigwa kwa kuiongoza lipuli.

"Umewahi wapi kusikia kiongozi anaongoza kwa kuwapiga wanachama wake huku akiwa anakiuka Katiba ya timu ya lipuli kwa kushindwa kulipa ada tu ya kuwa mwanachama hai wa lipuli". Alisema lonjino

Naye Katibu wa timu ya lipuli Wile Chikweo alisema kuwa  Chama cha mpira wa wilaya ndio chanzo cha migogoro hii inayoendelea kutokana na maslai yao binafsi hivyo wanapaswa kutafuta Njia ya kutafuta suluhu la mgogoro huu.

Chikweo alipngeza kuwa hutupingani na Chama cha mpira wilaya,Sasa hivi tunacheza mpira na tff taifa,tunasubiri muongozo kutoka tff juu ya migogoro iliyopo ndani ya lipuli inatatuliwaje.

"Mpaka sasa lipuli ina Wanachama wasiopungua 200 lakini tunakabisha mwanachama wapya ambao wakao kuwa wamekidhi vigezo vya kuwa wanachama hai,Hakuna kadi mpya zinatolewa zaidi yakufanya maombi yakuomba uanachama mpya ". Alisema Chikweo

Kwa upande wake Abu Changawe Majeki alianza kwa kuitambua iliyokuwa Kamati ya mipango na Fedha ya lipuli yarejeshwa rasmi kuendelea na kazi na kuwa kuanzia sasa msemaji mkuu wa lipuli atakuwa mwenyekiti wa Lipuli Fc kutoka na uzito wa mambo uliopo sasa na kuamuru aliyekuwa Msemaji wa timu Clement Sanga hapaswi kuongea chochote kuhusu lipuli kuanzia muda huo.

Aidha majeki alisema vikao vyote vinavyokaliwa na kamati tendaji ni batili kwa kuwa baadhi ya wajumbe hawakuwa na sifa na Baadhi ya wajumbe ambao hawana sifa yakuwa wajumbe..

Devota  MakamuMwenyekiti
Msomali
Andondile
Haruna

"Mpaka sasa siku ya Nne nipp Iringa sijapewa barua yakusimamishwa lipuli fc ndio ujue kuwa viongozi hao hawajui wanachokifanya na hawana uwezo wa kuwa viongozi maana wameshindwa kuiheshimu Katiba ya timu na inawezekana hata waijui Katiba yenyewe". Alisema Majeki

Uchagyzi utafanyika ndani siku 21 zijazo kuanzia leo na kuwaomba wadau wa lipuli watakutana Ijumaa uwanja wa Samora

Wakati huo huo kamati tendaji imesema kuwa inamtambua bwana Clement Sanga kama msema wa timu ya lipuli kwa kuwa hajafukuzwa kazi na uongozi na kuongeza kuwa Majeki hatumtambui Kabisa 

Asikatea kama barua hajapata kwa sababu tuliipeleka kwenye serikali yake ya mtaa kwa kuwa Abu Changawe Majeki akikutana na mjumbe yoyote wa kamati tendaji anwapiga hivyo njia sahihi ilikuwa kupeleka kwa Mwenyekiti wa mtaa.


Story hiii itaendelea kesho kwa kujua vitu vingi sana usikose kufuatilia

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More