Wednesday, May 25, 2016

MWIGULU CUP MBIONI KUANZA KUTIMUA VUMBI JIMBO LA IRAMBA

Mbunge  wa  jimbo la Iramba  Bw  Mwigulu Nchemba akikabidhi  vifa vya  michezo kwa  vijana  jimboni kwake  kwa  ajili ya  kuanza kwa kombe la Mwigulu jimboni humo
Vijana   wakipokea mipira  toka kwa Mwigulu Nchemba ambae ni mbunge wa  jimbo la Iramba na waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi  baada ya  kufanya  mikutano 9 ya  kuwashukuru  wananchi  wake
MBUNGE  wa  jimbo la  Iramba mkoani Singida   Mwigulu  Nchemba anakusudia kuzindua mashindano ya  kombe la Mwigulu  2016 litakaloshindaniwa na vijana  katika jimbo lake .
Nchemba  ambae ni  mmoja kati ya  mashabiki  nguli  wa  timu ya Yanga  alisema  kuwa  upo  uwezekano mkubwa  wa  michezo  kuendelea  kutoa ajira kwa  vijana  iwapo watajituma  zaidi katika mashindano hayo ambayo  yataanzishwa jimboni mwake kwa vijiji vyote  kushiriki .
Akikabidhi   vifaa vya michezo kwa timu mbali mbali za  vijiji 8 vya jimbo  la Iramba vikiwemo  vijiji  vya Mingela,Tulia ,Dolomoni ,Ntwike na vingine  wakati wa ziara  yake  ya  kuwashukuru wapiga  kura  wake ,alisema amekuwa  akifanya  hivyo  kila mwaka lengo ni kukuza  vipaji  vya vijana  ila kutoa  burudani baada ya kazi.
Nchemba  alisema  wilaya ya Iramba  na mkoa  wa Singida ni mmoja kati ya maeneo ambayo yanahistoria  kubwa katika soka la Tanzania na kuwa  wapo  baadhi ya  vijana wanachezea  timu  ya Simba wakiwa  wametokea  jimboni mwake na  hivyo upo  uwezekano wa  timu ya Singida United ambayo  imepanda  daraja kuweza  kupata  wachezaji wazuri  zaidi  kutoka katika mashindano  hayo.
Kwani  alisema kila  kijiji  kitashiriki  mashindano  hayo ya  Mwigulu  Cup na  kuwa wakati wa  mashindano wachezaji  wazuri  kutoka  kila  kijiji  watateuliwa  ili  kuunda  timu ya  wilaya kabla ya  kupata mchujo wa  wachezaji  watakaochezea timu ya  mkoa na nje ya  mkoa pale  inapowezekana.
Hata  hivyo alishauri  wachezaji  kucheza kwa nidhamu na kuacha  kugombana  wakati wote wa mashindano hayo na wakubali  kucheza  uwanja wa nyumbani na nje .

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More