Friday, May 6, 2016

HALIMASHAURI YA MJI WA MAFINGA YACHANGISHA WATUMISHI WAKE MADAWATI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga,Shaibu Nnunduma

NA RAYMOND MINJA MAFINGA.

Licha ya kuwa na rasilimali lukuki za mazao ya miti  kakini bado halmashauri ya wilaya Mafinga Mji inakabiliwa na uhaba wa madawati 2199 hali iliyolazimu halimashauri hiyo kuagiza watumisha wa serekali na madiwani changa kila mmoja dawati moja ili kukabiliana na uhaba huo

.
Hatua hiyo imekuja zikiwa zimebaki wiki kadhaa kwa wakuu wa mikoa kutekeleza na kukamilisha  agizo la Raisi Magufuli la kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi yoyote atakayekuwa anakaa chini katika mkoa
wake la sivyo mkuu huyo wa mkoa atawajibika juu ya swala hilo

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini mafinga juzi mwenyekjiti  mwenyekiti wa halimashauri hiyo Charles Makoga alisema kuwa wameamua kufikia uamuzi huo ili kumunga mkono Raisi Magufuli la kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayekaa chini wakati wa masomo .

Makoga alisema kuwa katika kutekeleza agizo hilo kila mfanyakazi wa halimashauri hiyo pamoja na madiwani kila mmoja atachangia dawati moja moja  hadai ifikapo mishoni mwa mwezi huo na yule ambaye hata tekeleza
agizo hilo basi ofisi hiyo itaangalia namna gani ya kumshungulikia .




“Tunatarajia kukusanya madawati Zaidi ya elfu moja na mia tano hivi kutoka kwa watumishi wetu pamoja na madiwani idadi hii ya madawati itasadia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatizo la madawati tusikimbilie kuwambia wazazi wachangie madawati wakati sisi hatuchangi tuanze sisi
na wao watafuata” alisema makoga

 Mkurugenzi wa halimashauri ya mji wa mafinga Shaibu Nnduma alisema itakuwa ni jambo la busara endapo watumishi wake watashiriki kikamilifu katika swala la uchangiaji wa madawati kwa hiyari yao ili
kuweza kumaliza tatizo hilo .

Ndunduma alisema kuwa halimashauri yake bado ni changa kwa kuwa haina fedha za kuendeshea miradi mbalimbali kutokana na kugawanywa kwa halimashauri hiyo kutoka halimashauri mama ya Mufindi hivyo kila mmoja anapaswa kuwajibika kwa kiasi kikubwa ili kuweza kumaliza changamoto za halimshauri hiyo likuwemo swala madawati

Naye diwani wa kata kata ya kinyanambo Chesco Lyuvale alisema kuwa uamuzi uliofikiwa na baraza hilo la madiwani  la kila mtumishi na diwani kuchangia dawati ni swala la kishuja na la kupongezwa kwani wanafunzi wanaoenda kukalia madawati hayo  katika shule hizo ni wa wazazi wote bila ya kuangalia kuwa ni mtoto wa tajiri , maskini aumuajiriwa wa serekali ,

“Hiii halimashauri imejaa rasilimali za kutosha ni aibu kuona mwanafunzi anakaa chini wakati sisi ndio tunaosifika kwa kutoa mbao kila kukicha itafika sehemu sasa unafika ugenini unaogopa kujitambulisha kuwa unatoka mufindi kwenye mbao kwa kuwa watakucheka
kuwa munamiti ya kutosha lakini bado watoto wanakalia mawe ”alisema lyuvale .

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa halimashauri hiyo anasema hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu watahakikisha tatizo la dawati katika halimashuri hiyo linapungua kama siyo kumalizika kabisa kwa kuwapitia wadau mbalimbali waliowekeza katika halimashauri hiyo ili na wao watoe
mchango wa madawati katika halimashauri hiyo .

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More