Tuesday, May 10, 2016

Bush Asema Hatampigia Kura Donald Trump

Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush amesema hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini humo Novemba mwaka huu.

Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.

‘‘Marais wa Marekani wanasifa zao na wanakubalika kwa watu, lakini huyu jamaa hana sifa hata moja ndiyo maana kila siku namkana na kusema hafai kabisa kuwa rais wa nchi hii, ’’alisema Bush

Jeb ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani kuwa hatampigia kura Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi ambayo imegawanya Chama cha Republican.

Juzi Spika wa Bunge, Paul Ryan alisema hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo tajiri ingawa atakutana naye wiki ijayo.

Hata hivyo, Trump aliungwa mkono na mgombea urais wa zamani wa nchi hiyo, Bob Dole aliyeshindwa katika uchaguzi na Bill Clinton wa Chama cha Democratic mwaka 1996.

Wiki iliyopita Seneta wa Texas, Ted Cruz alijitoa katika kinyang’anyiro cha kuwania uteuzi wa kugombea urais kwa Republican baada ya kushindwa katika uchaguzi wa awali dhidi ya mpinzani wake huyo.

Cruz aliwaambia wafuasi wake katika mji wa Indianapolis kwamba: “ Njia hii kuelekea ushindi imefungwa” na kusema kuwa wapiga kura wamechagua njia nyingine.

Alitoa shukrani kwa wafuasi wake wote. Trump alipata ushindi mkubwa Indiana huku Cruz akishika nafasi ya pili na gavana wa Ohio John Kasich akiwa katika nafasi ya tatu.

Trump alisema huo ni ushindi mkubwa kwake na kumpongeza Cruz akimuita yeye na wagombea wengine 15 waliokuwa wanagombea uteuzi wa Republican kuwa ni werevu na wenye nguvu.Alitoa wito wa kuwa na umoja ndani ya chama hicho.

Kwa upande wa Democratic seneta wa Vermond, Bernie Sanders ameshinda katika jimbo la Indiana dhidi ya Hillary Clinton

Wagombea hao wawili walibadilishana ushindi kabla ya Sanders kuibuka mshindi kwa asilimia saba ya kura. Hata baada ya ushindi huo wa Sanders katika jimbo la Indiana, Hillary anaongoza katika idadi ya wajumbe ikionyesha kwa mahesabu ni vigumu kwa Sanders kuteuliwa kuwa mgombea wa Democratic

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More