Tuesday, May 3, 2016

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Simon Berege, akitoa salamu za ufunguzi katika Maadhimisho ya Siku ya  Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.

Berege amesema Maadhimisho hayo yanafanyika huku wanahabari wakiwa wanapitia manyanyaso kutoka kwa vyombo vya dola, Wanasiasa na wakati mwingine kutoka kwa wananchi ambapo mwaka jana kuliripotiwa kesi 30 za manyanyaso kwa waandishi wa habari.

Ametoa rai kwa Serikali kufuta uamuzi wake wa kuzuia wananchi kupata habari, kwa kuzuia matangazo ya shughuli za bunge kuonyeshwa moja kwa moja (Live), huku akivisihi vyombo vya habari vya kijamii kurusha live vikao vya mabaraza katika halmashauri nchini ili kutoa fursa kwa wananchi kufuatilia bajeti za halmashauri zao.

Katika Maadhimisho haya, litazinduliwa Chapisho la Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika ambalo limeandaliwa na Misa Tanzania, chapicho hilo linaitwa "So This is Democracy"? (Je Hii ni Demokrasia).

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho haya ni Jaji Mkuu wa Tanzania ambae amewakilishwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba. Pia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nhauye pamoja na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Regnard Mengi wamehudhuria katika Maadhimisho haya.

Viongozi wengine wa Mashirika ya Kimataifa, Balozi mbalimbali, Taasisi Washirika, Wasomi wa Vyuo Vikuu pamoja na Wadau wengine wa habari wamehudhuria.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania akitoa salamu za ufunguzi katika Maadhimisho ya Siku ya  Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Mgeni rasmi Mhe.Robert Vicent Makaranga (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na wageni waalikwa wengine katika Maadhimisho ya Siku ya  Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Usia Nkhoma ambae ni Afisa Habari, Shirika la UN Infirmation Centre nchini Tanzania akitoa salamu zake katika Maadhimisho ya Siku ya  Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Zulmira Rodrigues ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa UN nchini Tanzania, akitoa salamu zake katika Maadhimisho ya Siku ya  Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika katika Maadhimisho ya Siku ya  Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More