Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa
faini ya Sh5 milioni kwa kila kosa waliokuwa Mkurugenzi wa Utafiti na
Mipango wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Samweli
Mvingira na Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Judith Msuya baada
ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia
Serikali hasara.
Hata
hivyo, mshtakiwa Judith Msuya ambaye alikuwa ni Naibu Mkurugenzi wa
Fedha na Utawala kutoka Mamlaka hiyo (Tan Trade) amelipa faini hiyo na
kuepuka kifungo cha miaka mitatu jela.
Washtakiwa
kwa pamoja wametiwa hatiani katika mashtaka manne kati ya matano
walioshtakiwa nayo mahakamani hapo likiwemo la kutumia madaraka yao
vibaya kwa kuagiza gari lililotumika kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya
Umma iliyosababisha AL Hamadi Motors FZD kupata faida ya Sh34. 89
milioni.
Katika
kesi hiyo, washtakiwa walikuwa watatu akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Tan Trade ambaye alifariki dunia wakati shahidi wa kwanza alipotoa
ushahidi wake.
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema ameridhishwa
na mashahidi wa upande wa Jamhuri ambao wameweza kuthibitisha mashtaka
dhidi ya washtakiwa hao.
“Nimewatia
hatiani washtakiwa hawa kwa makosa manne ya kutumia madaraka vibaya,
hivyo kosa la kwanza hadi la nne mtalipa faini ya Sh 5milioni kwa kila
kosa au kwenda jela miaka mitatu kwa kila kosa na shtaka la tano
nawaachia huru kwa sababu Jamhuri imeshindwa kuthibitisha shtaka hili,”
amesema Hakimu Mkeha.
Kwa
mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanadaiwa kuwa kati ya Septemba
2007 na Julai 2008, Makao Makuu ya TanTrade wilaya ya Temeke walitumia
madaraka yao vibaya kwa kuagiza gari lililotumika kinyume cha Sheria ya
Manunuzi ya Umma iliyosababisha AL Hamadi Motors FZD kupata faida ya
Sh34.89 milioni.
Katika
shtaka la pili, tarehe hiyo na mahali hapo, washtakiwa kwa kutumia
madaraka yao vibaya, walinunua gari iliyotumika kwa lengo la kumnufaisha
Humer Stars kiasi cha Sh32.77 milioni.
Katika
shtaka la tatu, washtakiwa wanadaiwa bila kufuata utaratibu wa
kushindanisha zabuni waliagiza gari iliyotumika na kusababisha AL Hamad
kupata faida ya Sh34.89 milioni huku shtaka la nne watuhumiwa walinunua
gari bila kufuata utaratibu wa zabuni.
Shtaka
la tano, ambalo washtakiwa waliachiwa huru baada ya Jamhuri kushindwa
kuthibitisha shtaka, washtakiwa walidaiwa kutumia madaraka yao vibaya,
uzembe na kumsababishia mwajiri wao hasara ya Sh49.145 milioni
0 comments:
Post a Comment