Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard
Kasesela anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya mwimbaji
wa nyimbo za Injili DR Tumaini Msowoya, katika ukumbi wa Highland Hall Iringa mjini.
Sambamba na kasesela wageni wengine
wa heshima kwenye uzinduzi huo ni Mbunge wa Jimbo la Iringa
mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa
kupita chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia
Abdalah, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha Baby Baraka Chuma na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali.
Akizungumza na blog hii DR Msowoya
alisema tayari albamu hiyo yenye nyimbo nane imeshakamilika.
“Naenda Iringa kurudisha shukrani
zangu kwao, nataka wajue nipo huku sio tu kwa sababu ya kazi bali huduma ya
kuimba niliyoanza ”
Alizitaja nyimbo zilizo kwenye albamu
hiyo kuwa ni Hakuna Matata, Mwamba, Amenitengeneza, Furaha, Mungu Mkuu,
Wanawake Jeshi Kubwa, Samehe na Mungu wa Rehema.
“Kazi hii nimeifanya chini ya
usimamizi wa JB Production ikisimamiwa na Producer Smart Bilionea Baraka. Ndiye
meneja anayesimamia kazi zangu kwa sasa,’ alisema Msowoya.
Lakini Meneja wa Dr Msowoya Smart
Bilionea Producer Baraka alisema tayari waimbaji na kwaya mbalimbali
kutoka Iringa na Dar es Salaam watamsindikiza kwenye uzinduzihuo.
Alizitaja kwaya zizothibitisha
kumsindikiza kuwa ni Wakorinto wa Pili kutoka Mufindi, Muhimidini na kwaya ya
Vijana kutoka Iringa mjini.
Baadhi ya waimbaji
ni Christopher Mwahangila anayetamba na wimbo wa ‘Mungu ni Mungu
tu’, Mchekeshaji na mwanamuziki mpya wa Injili Tumaini Martine maarufu kwa jina
la Matumaini wa Kiwewe, Christine Mbilinyi, Moses Simkoko, Ritha Komba na
Witness Mbise kutoka Dar es Salaam.
Wengine ni Rebecca Baraka, Jesca
Msigwa, Ester Mgunda, Rebecca Mwalingo, Dennis Lukosi, Wadi Mbelwa,
Peter Mgaya, Rehema Chawe, Twaibu Mgogo, Emma Sanga na Victoria Mwenda kutoka
Iringa.
“Waimbaji watakaomsindikiza ni wengi
nab ado tunaendelea kuwasajili wengine. Bado tupo kwenye mazungumzo na Bahati
Bukiku ambaye anaangalia ratiba yake, ikiwa sawa tutakuwa pamoja,”alisema.
Aliwatanzania kupokea kazi ya Msowoya
kutokana na ubora wake wa nyimbo zilizobeba ujumbe unaoweza kuisaidia jamii.
Historia
Hakuna Matata ni albamu ya pili ya
Msowoya baada ya ile ya kwanza ya Natembea kwa Imani kutofanya vizuri sokoni.
“Bahati mbaya niliitengeneza kutokana
na kiwango kidogo hivyo iliishia kabatini, namshukuru Mungu kwa sababu kazi hii
ni nzuri na wakazi wa Iringa wameipokea. Naamini itapokelewa kote,”alisema.
0 comments:
Post a Comment