Watanzania hii leo wanaadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia Oktoba 14,1999 akiwa nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu.
Lakini wakati huo huo katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, uliofunguliwa na Mwl.Nyerere mwaka 03.02.1980 kunafanyika tamasha la Mziki Mnene linaloandaliwa na EFM & ETV za Dar es salaam.
Katika tamasha hilo kuna matukio muhimu yanafanyika ambapo asubuhi tayari mazoezi ya viuongo (Jogging) pamoja na kumsaka mkali wa muziki wa Singeli yaani "Singeli Michano" yamefanyika. Mchana kutakuwa na mchezo wa soka baina ya kikosi cha EFM&ETV na timu ya Mwanza Veteran na jioni hadi kuchee itakuwa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
BMG imekusogezea mshindi wa Singeli Michano Mwanza #Live kutoka uwanja wa CCM Kirumba ambako tamasha hilo lililodhaminiwa na wadhamini kadhaa ikiwemo Biko, Cocacola na JB Fairmont Hotel linafanyika.
BMG Habari, Pamoja Daima!
0 comments:
Post a Comment