MBUNGE wa viti maalum, Ritta Kabati akizungumza na kamati ya shule na wazazi ambao hawapo pichani juu ya ukarabati wa shule ya Msingi Igeleke ambayo inakabiliwa na uchakavu wa majengo na miundo mbinu mibovu hali inayohatarisha afya na usalama wa wanafunzi na walimu.
Picha na Denis Mlowe
………………….
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MBUNGE
wa viti maalum mkoa wa,Iringa kwa tiketi ya CCM Ritta Kabati amechangia
kiasi cha mifuko ya saruji 100 na siling’ibodi 100 kwa shule ya msingi
Igeleke iliyoko katika manispaa ya Iringa kutokana na uchakavu wa
majengo ya shule hiyo.
Akizungumza
na kamati ya shule na wazazi wa shule hiyo mara baada ya kufanya
ukaguzi wa miundo mbinu ya shule hiyo mbunge Kabati alisema ni aibu kwa
shule kongwe kama hiyo kuwa miundo mbinu mibovu ambayo inawafanya
wanafunzi kukaa kwa wasi wasi.
Alisema
kuwa shule hiyo licha ya kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani
majengo yake hayaendani kabisa na hali halisi ya ufaulu wa wanafunzi
hivyo kwa kushirikiana na wazazi ambao wamechangia vitu mbalimbali
ukarabati wa shule hiyo utaanza jumamosi wiki hii.
Alisema
kuwa majengo ya shule hiyo yamechakaa hali ambayo inahatarisha afya na
uhai wa wananfunzi kwa kuwa vumbi kwa chini hivyo kutokana na hilo
atakahakikisha shule zote chakavu zinafanyiwa ukarabati uendane na ubora
unaotakiwa.
“
Nimetembelea shule nyingi mkoani kwetu hasa za msingi kuweza kuangalia
miundo mbinu na majengo yake kwa kweli hali inatisha na majengo mengi
yamekuwa chakavu hivyo nitajitahidi kwa kushirikiana na wadau wa elimu
kuweza kukarabati yaendane na hali ya sasa ya kuwa bora zaidi” alisema
Kabati
aliongeza kuwa shule ya Igeleke ni moja ya shule zinazofanya vizuri
katika mitihani yake lakini imeharika hovyo na inahitaji msaada wa
haraka kuikarabati kwa kuwa wanafunzi wanasoma katika mazingira magumu
na kudumisha elimu ya wanafunzi hao waendelee kuongoza mkoani hapa.
Hadi
sasa Kabati amekwisha fanya ukarabati kwa shule za msingi za Azimio,
Kihesa,Mtwivira na shule ya Kibwabwa ambazo alizitembelea na kubaini
uchakavu mkubwa wa majengo na miundo mbinu mibaya na shule nyingine
alizoahidi kuzifanyia ukarabati ni shule ya msingi Gangilonga.
0 comments:
Post a Comment