Tuesday, October 24, 2017

MSTAHIKI MEYA UBUNGO ZIARANI BARANI ULAYA KUSAKA MIRADI YA MAENDELEO

Mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,Ndugu Boniface Jacob.
yupo kwenye ziara ya kikazi Barani Ulaya kwa mwaliko wa JUMUIYA YA UMOJA WA ULAYA(European Union) yenye Makao makuu yake Brussels nchini Ubelgiji  iliyofadhiliwa na shirika la  Konrad Adenauer Stiftung

Mstahiki Meya atakuwa nje ya Ofisi kwa muda wa siku 10 kuanzia tarehe 22 October Mpaka tarehe 2 November atakapo rejea.

Ziara ina Maudhui na  Dhima kuu tano

1. Kuunganisha Halmashauri zinazoongozwa na Upinzani na mashirika ya kusaidia maendeleo ya bara la Africa chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

2. Kutafuta Fedha kwa ajili ya kusaidia jumuiya na vikundi katika sekta zisizo rasmi, viwanda vidogovidogo, wafanyabiashara wadogowadogo(wamachinga) n.k

3. Kuingiza Halmashauri katika Miji iliyosanifiwa na Mpango wa Miji endelevu katika Utunzaji wa Mazingira.

4. Kuanzisha Mpango wa mafunzo kwa Madiwani na Mameya wa upinzani namna ya kutatua changamoto zao bila utegemezi wa serikali kuu pamoja na kurusha maandiko katika ubao wa wafadhili wa Jumuiya za ulaya

5. Jumuiya ya Ulaya inafahamu ugumu wa kutoa ushirikiano endapo miradi italetwa kwenye Halmashauri za Upinzani, (Mwabepande compost plant,funded by Humburg council Gmb) at Kinondoni Mc,as case study

 Hivyo kuanzishwa Mpango wa fedha kwa Sekta binafsi katika kusaidia Miradi mikubwa ya Umma kusaidia kuruka viunzi vya Ukwamishwaji wa Miradi.

Mstahiki Meya ameshafika Makao makuu ya Jumuiya ya Ulaya 1040 Brussels-'BELGIUM na  amekutana na European Economic social committee(EESC) Na kukutana na Wakuu wa Utawala na vitengo Bw. Eric Ponthieu na Bw. Rafael Bellon Gomez ambao wamemkutanisha na Mashirika yote ya ufadhili wa miradi ya Maendeleo Barani Africa na kisha ataelekea ESSEN Rathaus Essen 
kwa Meya wa jiji la Essen na mkuu Idara ya Idara ya Miradi Bw. Mathias Sinn na baadae Berlin Campus Haus, kukutana na Bw.Wienfriend Weck, Mratibu wa sera za Maendeleo na Haki za Binadamu na kisha EUREF Campus na Kukutana na Dr Karlin Gerner ambaye ni Mkuu wa Mradi wa Miji endelevu.

Hamburg
Hamburg city,madam Inken Brus,mratibu wa Halmashauri ya jiji la Hamburg,Ujerumani

Baade ataelekea Instanbul city, I.C.L.EI office nchini Uturuki kabla ya Kurejea Nyumbani ,Tanzania,Ubungo Dar es salaam. ,  

IMETOLEWA NA
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More