Wednesday, October 11, 2017

KESI YA MSUKUMA NA MADIWANI NANE YAPIGWA TAREHE.

Mbunge wa Jimbo la Geita,na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoani Geita ,Joseph Kasheku(Msukuma) akiteta jambo  nje ya mahakama baada ya kesi kuhailishwa

Baadhi ya wananchi ambao walijitokeza kusikiliza kesi hiyowakiwa nje ya mahakama.


 Picha na Joel maduka.

Kesi inayomkabili Mbunge wa Geita na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mkoani Geita Joseph Kasheku Msukuma na madiwani nane imesogezwa mbele baada ya upande wa mashitaka kudai upelelezi haujakamilika.


Kesi hiyo ambayo ilikuwa isikilizwe leo imepangwa kutajwa tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu ambapo washitakiwa wote wapo nje kwa dhamana.


Kwa upande wake wakili anayewatetea washitakiwa Bw Deo Mgengeli ameelezea hatua ambayo imeendelea siku ya leo mahakamani hapo kuwa shauri limekuja na kwamba limetajwa na hadi sasa hakuna mshitakiwa ambaye ameongezeka hivyo mahakama imeamua tarehe Kumi mwezi wa 11 wawasili mahakamani kusikiliza tena kesi hiyo.


Aidha wakili Mgengeli amezungumzia suala la madiwani wengine waliokamatwa na jeshi la polisi na kutofikishwa mahakamani  amesema kuwa kukamatwa  kwa madiwani hao  ni jambo la kawaida  kwani ni swala la upepelezi kwa makosa ya jinai na kwamba alhamisi wanatakiwa kwenda tena polisi ili kujua ni kipi ambacho kinaendelea ila hadi sasa awana kosa lolote.



 Awali washitakiwa hao kwa pamoja walifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita Septemba 19 mwaka huu

Washitakiwa wanakabiliwa a mashitaka ya kufanya mkutano bila kibali, kuziba barabara na uharibifu wa bomba la maji linaloelekea kwenye mgodi wa dhahabu wa GGM.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More