Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya
ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga
Alumni Association wakiwa wanajadili kitu walipokuwa kwenye ziara ya kuitembelea shule waliyosoma
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya
ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga
Alumni Association wakiwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Tosamaganga mkoani Iringa
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya
ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga
Alumni Association wakiwa katika hospital ya Tosamaganga.
Na Fredy Mgunda,Iringa
Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya
ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga
Alumni Association wametoa msaada wa mashuka sabini na tano na vifaa tiba
vyenye thamani ya shilingi 1,672,500 katika hospitali ya Tosamaganga
iliyopo katika katta ya kalenga mkoani Iringa kwa lengo la kuendelea kuboresha
sekta ya afya ikizingatiwa kuwa wengi wao waliwahi kutibiwa hapo wakati
wanasoma.
akizungumza wakati wa hafla
ya kukadhi msaada huo mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association
ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya
mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi
alisema kuwa walijipanga kuja kutoa msaada huu kwa kuwa wangi wao walikuwa
wanatibiwa katika hospital hiyo wakati wakiwa masomoni miaka mingi iliyopita.
“Leo hii tunaafya njema kwa
ajili tulitibiwa vizuri kipindi tulivyokuwa tunaumwa na ilitusaidia kufanya
vizuri masomo yetu na ndio maana leo hii tupo hapa bila kupata huduma iliyobora
nafikiri wengi wetu tusinge kuwa hapa” alisema Mbilinyi
Mbilinyi alisema kuwa
wamechangisha kidogo walichopata wameamua kununua vifaa hivyo ambavyo
wanafikiri vitakuwa na msaada kwa wagonjwa waliopo hospitalini hapo.
“Hiki kidogo tu lakini
tunajua kwa namna moja au nyingine vinaweza kuwasaidia wagonjwa na kuwapunguzia
mzigo uongozi wa hospitali yetu pendwa ambayo imekuwa ikitutibu kwa muda mrefu
sana kipindi tukiwa masomoni katika sekondari ya Tosamaganga” alisema Mbilinyi
Dr Steven Biginagwa ni
daktari bingwa wa magonjwa ya watoto na mtafiti wa ugonjwa wa malaria alisema
kuwa hospital hiyo iliokoa maisha yake kwa kupata huduma bora kwani alikuwa na
ugonjwa wa utumbo kujifunga lakini
madaktari waliokoa maisha yangu hadi hii leo.
“Mimi nililazwa hapa mwezi
wa kwaza na mwezi wa pili wa masomo nilipata matatizo ya huo ugonjwa lakini
nashukuru mungu kuwawezesha wahudumu wote wa hii hospital kunitibu na kuokoa
maisha yangu hadi leo nipo na afya yangu njema na mfanyakazi niliajiliwa hivyo
bila kuwepo kwa hospital hii sijui leo hii ningekuwa wapi” alisema Dr Biginagwa
Dr Biginagwa alisema kuwa
licha ya kumaliza masomo yake lakini mitihani mine ya mwisho alifanyia hodini
akiwa amelazwa kutokana na ugonjwa aliokuwa nao na madaktari walimsaidia kupata
huduma bora ndio maana alifanya vizuri mitihani kwenye mitihani na kufaulu
vizuri.
“Kwa miaka yangu vyote
miwili nimekuwa nikishinda sana hapa hospitalini lakini mungu alisaidia
nikamaliza masomo yangu na nafikiri kutokana na hudumu nilikuwa napewa hapa
ndio iliyonipelekea kwenda kusomea udaktari na ndio maana hadi leo hii mimi ni
daktari bingwa wa magonjwa ya watoto” alisema Dr Biginagwa
Kwa upande wake mkurugenzi
mtendaji wa TASAF Ladslausi Mwamanga aliwaomba wananchi popote walipo hapa nchi
kukumbuka kutoa msaada waote katika hospital ili kuendelea kuboresha sekta ya afya
kwa kuwa serikali bila wadau haiwezi kukamilisha kila kitu yenyewe.
“Unajua kuwa serikali
inamambo mengi ambayo inayaofanya hivyo kukamilisha kila kitu kwa wakati ni vigumu
sana hivyo sasa sisi wadau tuendelee kuisaidia serikali kwa kile tuchokipata
kutoa msaada kwenye sekta hii ya afya ambayo inachangamoto nyingi sana” alisema
Mwamanga
Naye diwani wa kata ya
Kalenga Thobias Kangalawe aliwashukuru wanafunzi hao waliosoma shule ya
Tosamaganga miaka iliyopita kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya Tosamaganga,alisema
kuwa ni nadra sana kuona watu wanakumbuka walikopatia mafanikio na kutoa msaada
kama wenu.
Nyinyi watu wa kipekee
kabisa toka nimekuwa kiongozi siajwahi kuona kundi kubwa lenye kujali wapi
walikotoa na kuendelea kutafuta njia mbdala za kusiadia kutatua changamoto kama
nyinyi hivyo hongeni na namuomba mungu awaongezee pale mlipo punguza” alisema
kangalawe
0 comments:
Post a Comment