Sunday, October 15, 2017

KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA LAFANA MKOANI GEITA

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza wakati wa kongamano katika maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita wakifatilia kwa makini mada mbalimbali zikiwasilishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza wakati wa kongamano katika maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Mchambuzi na mshauri wa sera katika Wizara ya kilimo Ndg Revelian Ngaiza Akiwasilisha mada kuhusu mchango wa sera za kilimo katika mageuzi ya uchumi wa viwanda wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Meneja wa Muendelezo wa wakulima wadogo TADB Ndg Joseph Mabula Akiwasilisha mada kuhusu Mikopo nafuu kwa mapinduzi ya kilimo na viwanda wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa uendeshaji Mwandamizi Utoaji Mikopo na kudai madeni Kutoka Mfuko wa Pembejeo Ndg Joshua Kalab akiwasilisha mada kuhusu Mchango wa mfuko wa pembejeo katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kupambana na njaa na kupunguza umasikini hususani vijijini wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini kutoka Wizara ya Kilimo Ndg Issa Sabuni akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Katibu wa Chama cha Biashara Tanzania Mkoa wa Kagera (TWCC) Bi Paskazia Sebastian akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa Mfawidhi kutoka Taasisi ya udhibiti wa mbegu TOSCI Mkoa wa Mwanza Ndg Ngura Joseph Akiwasilisha mada kuhusu Mchango wa mbegu bora katika usalama wa chakula wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.


Afisa Kilimo Mkuu kutoka Wizara ya kilimo Bi Mwanaid Kiya Akiwasilisha mada kuhusu Sumu kuvu kwenye mahindi: Madhara katika sekta ya kilimo, Biashara na afya ya binadamu wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.

Na Mathias Canal, Geita

Zikiwa zimesalia siku mbili kufikia kilele cha maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambapo maadhimisho hayo huanza Octoba 10 kila mwaka na kufikia ukomo Octoba 16, wadau mbalimbali kutoka sekta ya kilimo na nyinginezo wameshiriki Kongamano la Maadhimisho ya chakula lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Katika kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga aliwasisitiza wataalamu wa kilimo kuwasaidia wakulima nchini ili kuongeza ufanisi katika kilimo kutoka katika kilimo kwa ajili ya chakula pekee badala yake na kuwa na kilimo tija kwa ajili ya chakula na biashara. 

Alisema kuwa ili kuongeza ufanisi na kukuza soko la mazao ya chakula na biashara nchini watanzania wanatakiwa Kuwa wazalendo na kupenda vyakula vitokanavyo na mazao mbalimbali yanayozalishwa nchini. 

Mkuu huyo wa Mkoa wa Geita aliwapongeza wadau mbalimbali walioshiriki katika Kongamano hilo ambao ni Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Vikundi vya wajasiriamali, Makampuni ya simu, na Shirika la umeme Tanzania TANESCO ambapo alisema kuwa imani yake kuwa kongamano hilo litaibua chachu katika uzalishaji wa kilimo na uhifadhi bora wa chakula.

Alisema kuwa umuhimu wa kongamano hilo unaakisi Kaulimbiu ya maadhimisho ya Chakula duniani kwa mwaka 2017 isemayo Badili mwelekeo wa uhamaji; Wekeza katika usalama wa chakula na maendeleo Vijijiniikiwa ni sehemu ya ubashiri wa kutokea mzozo mkubwa wa chakula.

Alisema jukumu muhimu la kilimo cha familia katika kuangamiza njaa na umaskini ni kuhakikisha kuna usalama wa upatikanaji wa chakula na lishe bora, kuboresha kipato, kusimamia vyema rasilimali, kuyalinda mazingira na kufanikisha maendeleo endelevu, hususani katika maeneo ya mikoani.

Katika Kongamano hilo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo Mada ya Mchango wa sera ya kilimo katika magaezi ya uchumi wa viwanda, Mikopo nafuu kwa mapinduzi ya kilimo na viwanda, Mchango wa mfuko wa pembejeo katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kupambana na njaa na kupunguza umasikini hususani vijijini.

Mada zingine rafiki katika kongamano hilo ni pamoja na Mchango wa mbegu bora katika usalama wa chakula, Umuhimu wa kilimo cha mazao ya mizizi kwa kuboresha lishe na kipato cha jamii, sumu Kuvu kwenye mahindi (Madhara katika sekta ya kilimo, Biashara na afya ya binadamu), Msingi wa uhuru wa kiuchumi na Tanzania ya Viwanda sambamba na Ufugaji nyuki unaoongeza mavunoya asali na kipato katika kaya.

Akiwasilisha mada kuhusu mchango wa sera za kilimo katika mageuzi ya uchumi wa viwanda Mchambuzi na mshauri wa sera kutoka Wizara ya kilimo Ndg Revelian Ngaiza Alisema kuwa Sera ya Taifa ya kushajiisha uwekezaji ya mwaka 1996 na Sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 imeiweka sekta ya kilimo kama sekta kiongozi katika uchumi hivyo Sekta hiyo imeendelea kuwa uti wa mgongo katika kukuza uchumi kwa kipindi cha kati na cha muda mrefu.

Alisema kuwa SerĂ¡ ya Taifa ya kilimo ya mwaka 2013 ilidhamiria Kuwezesha kuwepo mabadiliko ya sekta ya kilimo kuwa kilimo cha kisasa, kibiashara na sekta yenye ushindani ili kuhakikisha usalama wa chakula na upunguzaji wa umaskini kutokana na ongezeko la uzalishaji wa mazao yenye ubora.

Aliendelea kusema  kuwa katika Serikali ya Awamu ya tano kumekuwa na mikakati na programu mbalimbali ambazo zimetekelezwa na kuchangia kikamilifu katika kukuza kilimo na hifadhi ya jamii.  Alitaja programu na mikakati ambayo ni Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDS) wa mwaka 2002; na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II) ya mwaka 2006.

Ngaiza alisema Mabadiliko ya ukuaji wa sekta ya kilimo hadi kufikia kuchangia kwa kiasi kinacho ridhisha katika ukuaji wa uchumi wa Viwanda na upunguzaji wa umaskini bado kunahitajika juhudi za kila mdau miongoni mwao ni Serikali, wakulima, sekta binafsi, wanataalum n.k ili kutimiza azma hiyo.

Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Chakula Duniani hapa nchini Tanzania Kitaifa yatafikia ukomo tarehe 16 Oktoba 2017 katika Viwanja vya CCM Kalangalala, ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Dkt Charles Tizeba. 

Maadhimisho ya kwanza ya siku hii yalianza mwaka 1981. Hivyo maadhimisho ya mwaka huu ni ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na maadhimisho ya  miaka 72 ya kuanzishwa kwa FAO tarehe 16 Oktoba, 1945.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More