Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta kuu za
matumizi ya Ardhi na Asasi za Kiraia wamekutana kwa ajili kuendelea kurejea
Mwongozo wa ushirikishaji katika kupanga mipango ya matumizi ya Ardhi pamoja na
kukamilisha kazi ya rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto
zinazoikabili mipango ya matumizi ya ardhi ikiwemo kuutafsiri kwa lugha ya
kiswahili.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi
ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi, pamoja na kupongeza kazi nzuri ambayo
inafanywa na kikosi kazi, lakini pia lizungumzia swala la mipango
miji,upangaji wa mipango bora ya matumizi ya ardhi utakaozingatia
mtazamo wa kuipeleka nchi katika Dira ya viwanda na pamoja na swala la mabadiliko ya Tabianchi, ili wananchi wawe tayari
kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabianchi kunatakiwa kuwe na
mipango mizuri ya matumizi ya ardhi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uratibu, Sera na Mawasiliano wa TumeBi. Albina Burra akitoa maelezo mafupi kwa Mkurugenzi wa Tume
hiyo Dkt. Stephen Nindi kuhusiana na kazi kazi ya kikosi kazi ya
kukamilisha andiko la Mkakati wa changamoto za mato za matumizi ya Ardhi
ikiwa ni pamoja na kuandaa mwongozo na kubadili andiko kwa lugha ya
kingeleza ili lipate kusomwa na wafadhiri pia wadau wengine.
Afisa
Mipango kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Gerald
Mwakipesile (wa kwanza kulia) akiwapitisha kikozi kazi katika maeneo
mbalimbali ya kukamilisha mkakati wa kutatua changamoto za matumizi ya
Ardhi nchini.
Afisa
Tawala wa Tume ya Taifa ya Mipango ya matumizi ya Ardhi Bi. Nakivona
Rajabu akitoa mrejesho wa kikao kilichofanyika na Mh. William Lukuvi
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokuwa anakabidhiwa
Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya Ardhi cha
tarehe 14.08.2017 mjini Morogoro.
Wanakikosi kazi wakiwa wanafuatilia mrejesho huo
Wanakikosi
kazi wakiwa katika makundi kwa ajili ya kushirikiana kwa pamoja
kulibadili andiko la mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya
Ardhi kwa lugha ya kingeleza ili uweze kuja kusomwa na wafadhiri pamoja
na wadau wengine mbalimbali.
Bw. Emmanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, akitoa maoni yake wakati wa mkutano huo.
Bwana Daniel Ouma(kushoto) Afisa Miradi kutoka TNRF akichangia jambo wakati kikosi kazi kikiendelea na kazi.
Bw.
Mbaraka Stambuli kiongozi wa Kipengele cha maendeleo ya kisera na
kitaasisi katika programu ya kuwezesha umilikishwaji wa Ardhi,
akichangia jambo la maboresho wakati wa kubadilisha andiko katika lugha
ya kingeleza.
Bwana
Herman Nyanda Afisa wanyama pori (TAWA) mwandamizi katika dawati la
ushirikishwaji jamii katika uhifadhi wa wanyama pori akichangia hoja
wakati shughuli ya kubadilisha andiko katika lugha ya kingeleza
inaendela
Kikosi kazi wakiendelea na kazi
0 comments:
Post a Comment