Mbunge
wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa
amefunguka na kusema kuwa biashara ya kununua madiwani wa CHADEMA pia
ilifanyika Iringa na kusema kuwa wao walitumia vifaa kutoka Australia
kubaini hilo.
Peter
Msigwa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kutoka Ofisi za
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo walikwenda
kuwasilisha ushahidi wa Rushwa dhidi ya kununuliwa kwa madiwani hao na
wateule wa Rais John Pombe Magufuli.
"Iringa
mjini biashara nayo ilifanyika na nina ujasiri mkubwa kwamba muhusika
mkuu wa biashara ya kununua madiwani Iringa Mjini ni ofisi ya Mkuu wa
Mkoa, Mkuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya polisi.
"Hiyo mliona 'Episode' ya Arusha vilitumika vifaa vya Uingereza kule Iringa tulitumia vifaa vya Australia na sisi tutafungua jalada kama ambavyo Mkurugenzi wa TAKUKURU ametushauri kwa hiyo tusubiri sababu tumekabidhi kwenye korido za serikali na tunataka sheria zichukue mkondo wake huu uongo uongo wa kusema watu wanaunga mkono utendaji wa serikali tunataka ufike mwisho ili watu wakae kwenye nafasi zao kwa haki na jinsi ambavyo watu waliamua kuwachagua" alisema Msigwa

0 comments:
Post a Comment