Monday, October 30, 2017

DKT MWANJELWA ATUA ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO WA TFA

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwingine ni Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza kwa makini maelezo ya hali ya Upatikanaji wa Chakula kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akijadili jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro wakati akiondoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwingine ni Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Rasilimali watu (Utawala) wa Mkoa wa Arusha.

Na Mathias Canal, Arusha

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 27, 2017 aewasili Mkoani Arusha Kwa Ziara ya kikazi ambapo kesho Octoba 28, 2017 atafungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA).

Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha utahudhuriwa na viongozi mbalimbali huku ukitaraji kuhudhuriwa na Wanachama wa Tanganyika Farmers’ Association (TFA).

Pamoja na mambo mengine mkutano huo utabainisha vyema kazi na Huduma zinazotolewa na TFA ambazo ni kuuza Zana bora za kilimo, Pembejeo za kilimo kama Mbolea, Mbegu bora, Viuwatilifu mbalimbali pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa Wakulima, kama juhudi ya kumpunguzia mkulima karaha ya upataji wa huduma hizo,

TFA ni mojawapo ya Taasisi kongwe na muhimu kwenye maendeleo ya Sekta ya Kilimo nchini Tanzania na imekuwa ikihudumia Sekta hiyo kwa miaka zaidi ya 80 sasa, tangu ilipoanzishwa mnamo mwaka 1935.

Aidha, Kampuni ya TFA imekuwa ikifanya kazi na Serikali kwa njia ya kutoa huduma kubwa kwa Wakulima wote nchini pale ambapo TFA ina matawi ambayo husambaza na kuwafikishia Wakulima, pembejeo za kilimo zenye ubora wa hali ya juu, kwa wakati na kwa bei nafuu.

MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More