Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa MWL. Zawadi Mgongolwa akizungumza wakati wa mkutono mkuu wa chama hicho manispaa ya Iringa katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa
Meza kuu wakiimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wliaya ya Iringa manispaa
baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano mkuu wa chama hicho
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Chama cha walimu Tanzania (CWT)
wilaya ya Iringa manispaa wameulalamikia utaratibu wa maafisa elimu kuwanyima
ruhusa walimu kwenye matukio muhimu ya kitaifa na kwenye shida binafsi ambapo
husababisha kushuka kwa morali ya kufundisha wanafunzi.
Akizungumza wakati wa
mkutano mkuu wa chama hicho mwenyekiti wa manispaa ya Iringa MWL. Zawadi
Mgongolwa aliwatupia lawama maafisa elimu na walimu wakuu wa shule kwa
kuwanyima ruhusa bila kuwa na sababu maalum.
“Mkurugenzi amekuwa ametoa
kibali upewe ruhusa lakini viongozi waliochini ya mkurugenzi wanatuwekea
vipingamizi ambavyo havieleweki kitu kinachozua utata mkubwa baina ya viongozi
na walimu ambao sio viongozi” alisema Mgongolwa
Mgongolwa alimpongeza mkurugenzi
wa halmashauri ya manispaa ya Iringa kwa kuwajali walimu kwa kuwapa ruhusa pale
inapotakiwa tofauti na hali ilivyo kwa hawa viongozi wa chini yake.
“Unakuta siku ya wanawake
duniani au siku ya walimu duniani bado walimu wananyimwa ruhusa wakati muda huo
mkurugenzi amewaruhusu walimu kuhudhuria sherehe hizo kitu kinachoongeza ukakasi
baina ya watendaji wa nafasi za juu na watendaji wa nafasi za chini” alisema Mgongolwa
Aidha Mgongolwa alisema kuwa
viongozi wa walimu wamekuwa wakipokea kero hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu
kwa kushindwa kutafutiwa ufumbuzi hadi leo hii.
“Unajua mwalimu akikosa
ruhusa huwa anajisikia vibaya na akitoka hapo sina uhakika kama mwalimu ataenda
kufundisha vizuri kwa kuwa atakuwa tayari akiri yake ilikuwa kupata ruhusa ili
aende akatatue matatizo yake” alisema Mgongolwa
Mgongolwa aliwapongeza walimu
wa manispaa ya Iringa kwa kuendelea kufanya kazi kwa kujituma licha ya
kukumbana na changamoto mbalimbali ikiwepo kunyimwa ruhusa.
Akijibu hoja hiyo katibu
tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka alisema haelewi kwanini mara kwa
mara swala hilo linakuwa linajirudia maana tulishalitafutia ufumbuzi hapo awali.
Sasa naenda kuandika barua
rasmi kwa mkurugenzi ili kutatua kabisa tatizo hilo maana hata kwangu imekuwa
kero na mwazoni nilijua wakuu wa shule ndio tatizo kumbe maafisa elimu ndio
tatizo naenda kulishughulikia kwa haraka sana swala hili” alisema Chintinka
Chintinka aliwataka maafisa
elimu na wakuu wa shule wote wa wilaya ya Iringa kuwapa ruhusa walimu pale
ambapo wanapata matatizo maana hakuna haja ya kumnyima ruhusa mtu akiwa
anashida na watakiwa kuzifahamu siku za kitaifa ambazo ni lazima walimu wahudhurie
wanapaswa kutoa ruhusa bila kipingamizi.
“Kunasiku kama siku ya
mwalimu,siku ya wanawake na siku nyingine za kitaifa walimu wanapaswa kupewa
ruhusa kwenda kuhudhuria tukio hilo kutokana na umuhimu wake” alisema Chintinka
Chintinka alisema kuwa
mkurugenzi ndio mwajili sasa hao maafisa elimu na wakuu wa shule wanatoa wapi
hiyo jeuri ya kuwanyima ruhusa ambayo viongozi wa ngazi za juu wanajua kuwa
kunakitu kinafanyika cha taifa.
Naye afisa elimu wa shule za
msingi manispaa ya Iringa Samweli Mtovagakye alisema kuwa watawatafuta hao
maafisa ambao wanawanyima ruhusa walimu wakati swala hilo lilishatafutiwa
ufumbuzi.
“Jamani sisi huku sheria
tulishaiweka kwenye matukio muhimu ya kitaifa walimu wapewe ruhusa sasa sijui
ili sawala limetoka wapi naomba nikitoka hapa nitazungumza na wakuu wa shule
pamoja na maafisa elimu wenzangu” alisema Mtovagakye
Mtovagakye aliwaomba walimu
wampe muda ili aweze kulichunguza upya kwa nini swala hilo linajirudia mara kwa
mara wakati walishalizungumza.
0 comments:
Post a Comment