Monday, October 16, 2017

DC MTATURU: TUMUENZI MWALIMU NYERERE KWA VITENDO VINAVYOACHA ALAMA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwagawia chai na vitafunwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko Mara Baada ya kutembelea Shule hiyo wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 18 ya kifo Cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko Mara Baada ya kutembelea Shule hiyo wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 18 ya kifo Cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage NyerereMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisafisha mtaro pembezoni mwa kituo Cha Afya Ikungi wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 18 ya kifo Cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage NyerereBaadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko wakifurahia ugeni wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kushiriki nao Hafla ya kumbukizi ya miaka 18 ya kifo Cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiteta jambo na Moja ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko Mara Baada ya kutembelea Shule hiyo wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 18 ya kifo Cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage NyerereMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza Jambo Mara bada ya kukamilika kwa mazoezi ya viuongo kabla ya kuanza zoezi la kufanya usafi katika Maeneo mbalimbali Wilayani humo wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 18 ya kifo Cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Na Mathias Canal, Singida

Leo Octoba 14, 2017 Watanzania wote Ulimwenguni wameungana kwa pamoja kumuombea kheri na Mapumziko yenye Amani Muasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki Dunia Miaka 18 iliyopita.

Ni ukweli usiopingika kuwa Watanzania kote Dunia wanakumbuka Wema, Busara, Upendo, amani, hekima na ucheshi wa  Mwalimu Julius Nyerere ikiwa Ni pamoja na Uongozi wa kuthubutu na kuacha alama.

Wakati maombi hayo yakifanyika Kitaifa Mkoani Kaskazini Unguja Visiwani Zanzibar na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuambatana na shughuli ya uzimaji Mwenge Kitaifa, katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kumbukizi hiyo imekuwa ya aina yake na tija kwa Uongozi wa Wilaya na wanachi kwa ujumla kushiriki shughuli za Kijamii ikiwa Ni pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewaongoza Mamia ya wananchi katika kumbukizi ya kifo Cha Baba wa Taifa kwa kufanya usafi katika kituo Cha Afya Ikungi na kushiriki mlo wa asubuhi (Chai) na Watoto walemavu ambao Ni wanafunzi wa shule ya Msingi mchanganyiko Ikungi.

Akizungumza na wanafunzi hao Mara Baada ya kushiriki nao kunywa chai Mhe Mtaturu Alisema kuwa hiyo Ni Sehemu ya faraja na kuonyesha upendo kwao kwa  kumuenzi Mwalimu JK Nyerere kwani aliewapenda watanzania wote kwa uzalendo wake katika Taifa, Uadilifu na Uaminifu Jambo ambalo viongozi wote wanapaswa kuiishi misingi hiyo ya haki na wajibu.

Mwalimu Nyerere aliamini katika nguvu ya umoja na mshikamano baina ya nchi na nchi. Kutokana na ujasiri, ushupavu na nia ya dhati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume walibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964 na hivyo kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliohusisha Muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar.

Alisema kuwa Hayati Mwalimu JK Nyerere alijenga nchi ya Tanzania katika misingi ya ujamaa na kujitegemea, alijenga mashirika ya umma, umoja na mshikamano wa kitaifa huku akipinga vikali masuala ya ukabila, udini, ubaguzi na rushwa.

Katika Hatua nyingine alipokea taarifa ya wanafunzi hao iliyobainisha changamoto za shule ikiwemo upungufu wa mabweni, Vyumba vya madarasa, Vifaa vya kufundishia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, Magodoro na vyombo maalumu kwa ajili ya chakula taarifa  iliyoambatana na pongezi kwa juhudi mbalimbali anazozifanya za kuleta maendeleo ya wananchi na jamii yenye mahitaji maalumu katika Wilaya ya Ikungi na Taifa kwa Ujumla wake.

Mhe Mtaturu aliwahakihakishia wanafunzi hao maombi yao waliyoyawasilishi kwake mwaka jana kuhusu kupatiwa mashine ya kuchapishia mitihani ya wanafunzi wasioona (Thermalform Machine) huku aliwaeleza jinsi alivyoanza utekelezaji kwa kuiomba Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) ambapo walikubali kutoa jumla ya Shilingi Milioni 45 ili kununua Mashine hiyo Sambamba  na vifaa vinginevyo atakavyo wakabidhi hivi karibuni baada ya taratibu za manunuzi kukamilika.

Aidha, Mhe Mtaturu alikubali ombi la kuwatafutia magodoro 105 huku akiwaahidi kwapatia Ng'ombe wa maziwa ili uwe mradi wa Shule kusaidia huduma za wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Akizungumza kwa niaba ya walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko Mwalimu Leonard Adamu alimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuboresha elimu Wilayani humo huku akiunga mkono kampeni ya Uboreshaji elimu kupitia Mfuko wa Elimu inayoendeshwa kwa kuwahusisha wananchi wote.

Alisema Ni wazi kuwa Historia imeandikwa kwani sio Jambo jepesi kwa kiongozi mkubwa kama Mkuu wa Wilaya kutenga muda wake kunywa chai na wanafunzi Sambamba na kushiriki Huduma za Kijamii ikiwemo kufanya usafi katika Maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Ikungi.

Naye Mkuu wa shule hiyo ya Msingi Ikungi Mchanganyiko Mwalimu Ibrahim Kulaya pamoja na mambo mengine aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli Kwa juhudi kubwa inazozifanya za kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kote nchini.

Alisema Mhe Rais Dkt Magufuli anafanya kazi kwa weledi mkubwa huku juhudi zake za kulinda rasilimali za nchi zikiwa ni njia sahihi ya kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo kutokana na matendo makubwa na muhimu katika Taifa aliyokuwa anayafanya wakati wa Uhai wake.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa Aprili 13, 1922 kijijini Butiama Mkoani Mara ambapo enzi za Uhai wake  aliamua kuiacha kazi yake ya Ualimu na kuingia kwenye mapambano makali ya kusaka Uhuru wa Tanganyika ambapo jitihada zake za dhati zilizaa matunda Disemba 9, 1961 kwa kupata Uhuru toka kwa Waingereza.

MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More