Mafundi wakiratibu zoezi la ukarabati wa mshine |
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco), limefanikiwa kukarabati
mashine namba 6 iliyokuwa imeharibika na kuiwasha kwa ajili ya kutoa huduma ya
umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Hatua ya kuwashwa kwa mtambo huo ni juhudi za shirika hilo
za kuimarisha hali ya upatikanaji umeme kwa wananchi kusini huku ikiwa ni
siku moja baada ya Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alipotembelea
Kituo cha kufua umeme kwa gesi .
Akizungumza leo mjini hapa, Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco,
Mhandisi Dk. Tito Mwinuka ambaye amepiga kambi mkoani humo pamoja na watalaamu
wengine, alisema kuwa mitambo iliyokuwa ikifanya kazi ilikuwa minne lakini
baada ya juhudi kubwa za wataalamu wa Tanesco hadi kufikia jana jioni
wamefanikiwa kuwasha mashine hizo zenye uwezo wa kuzalisha Megawati 16.
“Tanesco tumeshagiza vipuri vya aina mbalimbali ili
kutengeneza mashine hizi na pia Shirika katika kuhakikisha kazi inakwenda kwa
kasi zaidi itaongeza nguvu ya wataalamu kutoka vituo vingine vya TANESCO hapa
nchini.
“Tunawaomba wateja wetu wa mikoa ya Lindi na Mtwara
kuendelea kuwa wavumilivu wakati uongozi wa Shirika, Kanda na Mkoa ukiendelea
na juhudi za kumaliza kabisa upungufu wa umeme katika mikoa hii,” alisema Dk.
Mwinuka.
Alisema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya umeme kwa
mikoa hiyo, alisema Shirika limeshaanza taratibu za kupata Megawati nne za
haraka kwa kuagiza mitambo mwili mipya.
“Tuna imani kubwa na wafanyakazi wa Kituo cha kufua umeme wa
gesi cha Mtwara na wataweza kukarabati mitambo yote pindi vipuri
vitakapowasili,” alisema
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo amewashukuru wananchi wa
mikoa ya Lindi na Mtwara kwa uvumilivu waliouonesha katika kipindi cha
matengenezo ya mitambo hiyo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Tito Mwinuka, (wakwanza kushoto), na viongozi wengine wa Shirika hilo, wakifuatilia maendeleo ya ukarabati wa mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara leo Oktoba 17, 2017.
Mafundi wa TANESCO wakiendelea na ukarabati wa mshine.
0 comments:
Post a Comment