Afisa mtendaji wa kata ya Ng’ang’ange bwana Aron Mwenzegule akiwa mjumbe wa mkutano mkuu
taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela wakibadilisha mawazo wakati wa ziara ya kutembelea shule ya msingi Mdeke
Mwalimu mkuu wa shule ya Mdeke Pascal Aloyce akizungumza mbele ya wajumbe wa chama cha mapinduzi wakati wa ziara ya kubaini changamoto za shule hiyo
Mjumbe wa mkutano mkuu
taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela akiwa makini kusikiliza anachoambiwa na mwalimu wa shule ya msingi Mdeke wakati wa ziara yake katika shule hiyo.
Na Fredy Mgunda,Kilolo.
Shule ya msingi ya Mdeke
iliyopo kata ya Ng’ang’ange wilayani kilolo ina walimu 6 wanaowafundisha zaidi
ya wanafunzi 440 na kusababisha kutotolewa kwa elimu bora kwa wanafunzi
wanaosoma katika shule hiyo.
Hayo yamebaini wakati wa ziara
iliyofanywa na wajumbe wa kati za siasa wa
chama cha mapinduzi (CCM) wilayani
kilolo walipokuwa wameenda kwa lengo la kufanya usafi katika kata ya Ng’ang’ange
Akizungumza mara baada ya
kumaliza kufanya usafi mwalimu mkuu wa shule ya Mdeke Pascal Aloyce alisema kuwa
shule inajumla ya walimu 9 lakini walimu walimu watatu wameenda kusoma hivyo
walimu waliopo shuleni ni walimu sita na kusababisha ugumu wa kuwafundisha wanafunzi
wa shule hivyo.
“Tuna jumla ya wanafunzi 448 na
walimu tupo 6 sasa utaona kiasi gani tunapata ugumu wakufunzisha wanafunzi na
kuwapa elimu bora kwa kuwa walimu tumezidiwa na idadi ya wanafunzi huku walimu
wengine wakifundisha masomo ambayo hawayawezi vizuri” alisema Aloyce
Aloyce alisema kuwa licha ya
kuwa kuna walimu sita lakini walimu wawili wanafundisha elimu ya awali na
walimu wanne ndio wanafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba hapo ndio
utakundua kiasi gani kazi ya ualimu katika shule hii inakuwa ngumu.
“Ukiangalia tuna madarasa saba
hivyo walimu wanne tu ndio tunafundisha hapo utaona kwa kiasi gani tunapata
ugumu wa kufundisha na kuwapa elimu bora wanafunzi wetu hivyo tunawaomba
mtufikishie kilio chetu huko juu ili kuweza kutatua tatizo hili” alisema Aloyce
Aidha Aloyce alisema kuwa
walimu wa shule hiyo wamekuwa wakijitoa kufundisha kwa jitihada zao zote na
kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi wanasoma katika shule hiyo licha ya kuwa na
changamoto lukuki.
“Ukingalia mwaka huu tulikuwa
na wanafunzi 53 na waliofaulu ni wanafunzi 40 hivyo utagundua kwa kiasi gani
sisi walimu wa shule hii tunahitaji pongezi kwa kazi tunayoifanya licha ya
changamoto zinazotukabili walimu wa shule hii ya Mdeke” alisema Aloyce
Lakini Aloyce alisema kuwa
walimu wanakumbana na changamoto ya nyumba za walimu hivyo inawalazimu walimu
kuishi umbali wa zaidi ya kilimeta mbili hadi ufike shule hivyo utaona kuwa
walimu mara kwa mara wanafika shule wakiwa wameshachoka na kuathiri swala la
ufundishaji wanafunzi.
“Mwalimu anatoka mbali sana sasa
unafikiri mwalimu huyo akifika shule inakuaje hivyo na hii changamoto tunaomba mtupelekee
huko kwa viongozi wa ngazi za juu mfano tunawalimu anayenyonyesha hebu angalia
mwalimu hadi anyonyeshe unafikiri atafika shule saa ngapi tatizo la nyumba ni
kubwa sana” alisema Aloyce
Kwa upande wake mjumbe wa
halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo Saidi Kiponza alisema
kuwa wameziona changamoto zilizopo katika shule hiyo na kwenda kuzifikisha kwa
viongozi wa ngazi za juu ili kuweza kuzitafutia ufunzi na kwafanya wafanyakazi
wa serikali kuitekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kikamilifu.
“Sisi hatujaja kwa maonyesho
tumekuja kufanya kazi na kuhakikisha viongozi wa serikali wanaitekeleza vilivyo
ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020 ili chama hiki kiendelee
kuwa madarakani miaka yote” alisema Kiponza
Naye mjumbe wa mkutano mkuu
taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela alisema kuwa lengo la ziara
hiyo katika kata ya Ng’ang’ange ni kufanya usafi na kubaini changamoto
zinazowakabili wananchi na kuzipeleka
kwa viongozi wa serikali kuzitafutia ufumbuzi wa changamoto ambazo tunakuwa
tumezibaini na kuzitatua.
“Unajua ukujua eneo gani
kunachangamoto gani inakuwa kazi rahisi sana kuzitafutia ufumbuzi mapema na
kuwafanya wananchi waendelee kukiamini chama cha mapinduzi kwa kazi yake
inayofanywa chini ya Rais wetu Dr John Pombe magufuri kwa kazi kubwa
anayoifanya ya kuleta maendeleo” alisema Gervas Kahemela.
Usikose kutembelea blog hii kwani bado kuna habari ya kuhudhunisha kutoka katika shule hii ya Mdeke ilyopo wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.
0 comments:
Post a Comment