Friday, October 6, 2017

DC MTATURU AKUTANA NA WATAALAMU WA KILIMO IKUNGI KUJADILI UBORESHAJI SEKTA YA KILIMO

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira.
Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao cha kazi
 Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
 Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
 Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo (Aliyesimama) akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Mwingine ni Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Katikati), Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo (Kulia), Mwingine ni Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekutana na kufanya kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira kubaini kwa pamoja mbinu bora za kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao ya chakula na biashara kwa wingi.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Maafisa kilimo na Mifugo, Maafisa Ardhi, Maliasili na Mazingira, Maafisa Ugavi wa Kata sambamba na Maafisa Tarafa, Mhe Mtaturu alisema kuwa bado uzalishaji wa mazao ni mdogo katika Wilaya ya Ikungi ukilinganisha na hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kuwa na ardhi nzuri.

Aliwataka wataalamu hao wa kilimo kuwasaidia wakulima ili kuiwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kuwa kilimo cha kibiashara kitakachowezesha kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kupunguza umasikini kwa watanzania Sambamba na kujitosheleza kwa chakula. 

Mhe Mtaturu alisema Ili kuwe na kilimo kizuri na tija kwa wananchi, Wataalamu mnapaswa kuzingatia uwepo wa Pembejeo za kilimo na mbegu Bora za kisasa ambazo zinazalisha mazao mengi sambamba na kuhuisha kilimo cha umwagiliaji kwa kuandaa mpango wa kujenga skimu za umwagiliaji ili wananchi waweze kuzalisha chakula cha kutosha mwaka mzima.

Alisema kuwa ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo tayari serikali imetoa tani 20 za mbegu za Pamba katika Wilaya ya Ikungi ambazo zitagawanywa kwa wakulima ili msimu wa kilimo unapoanza tayari ukata wa kucheleweshwa kwa mbegu hizo uwe umetekelezwa.

Pia aliwaagiza maafisa ugani kuwa na mashamba darasa kwani kupitia wao yatawasaidia wakulima kuwa na uelewa mkubwa katika kuongeza ufanisi wa kilimo chenye tija.

Aidha, Alisema kuwa Katika kutekeleza majukumu ya wananchi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanzisha huduma zake kanda ya Kati Dodoma kwa kulenga mnyororo wa ongezeko la thamani katika mazao ya kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania. 

Mhe Mtaturu alisema ni vyema kama Wataalamu wa Kilimo watatumia nafasi hiyo kuwaunganisha wakulima na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo.

Katika kikao hicho Cha kuwakumbusha majukumu wataalamu hao Mhe Mtaturu amewataka kuandaa mpango kazi wa mazao ya Kilimo hususani mazao ya chakula na Biashara.

Mhe Mtaturu aliwaelekeza wataalamu hao wa kilimo kuwasisitiza wananchi katika maeneo yao kuanza kulima mazao ya kipaombele yaliyoelekezwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa ambayo Ni zao la Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.

Alisema pomoja na mazao hayo ya kipaumbele lakini pia wananchi wanapaswa kuendelea kuongeza nguvu katika mazao yanayostawi kwa wingi Wilayani humo ikiwa Ni pamoja na zao la Alizeti, Mtama, Mahindi na zao la Dengu.

Katika upande mwingine Mhe Mtaturu alishauri wataalamu wa Mifugo kutilia msisitizo Ufugaji wa kisasa (Ziro Grazing) kwa kutembelea na kupata utaalamu wa Ufugaji na mbegu Bora za ya Ng'ombe wa kisasa kwa wataalamu katika Rachi ya Taifa ya Kongwa (NARCO) na LITI iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya aliagiza heka 1500 ambazo ni kichaka kuandaliwa utaratibu kwa ajili ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa kilimo.

Naye Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo alipongeza kasi ya uwajibikaji ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa ufanisis wake katika uwajibikaji na kusaidia kuonyesha njia jambo ambalo linapelekea kubadili fikra za wakulima na wananchi kwa ujumla.

Sengo Alimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi kwa kuwezesha kupatikana muwekezaji ambaye atapewa heka 1000 Na serikali ya kijiji kwa ajili ya kilimo cha korosho zao ambalo litakuwa na tija kwa pande zote mbili kwani pia wananchi watanufaika na huduma za ugani na kuweka mkakati wa namna kijiji kitakavyonufaika na uwekezaji huo.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More