mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM manispaa ya
Iringa Said Rubeya akizungumza na wanachama wa chama hicho wakati wa kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo manispaa ya Iringa akiwa sambamba na viongozi wa chama katika ofisi za CCM wilaya pale sabasaba.
Edwin bashir ni katibu wa
chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa akiwa na Baraka Kimata aliyekuwa katibu mwenezi na Diwani
wa kata ya Kitwiru ambaye amejiunga rasmi na CCM pamoja Raymond kimata
aliyekuwa kiongozi wa redbrigad manispaa ya Iringa na katibu mwenezi wa kata ya
kitwiru naye kajiunga na CCM
Baraka Kimata aliyekuwa katibu mwenezi na Diwani
wa kata ya Kitwiru ambaye amejiunga rasmi na CCM akionyesha kadi ya mpya ya chama cha mapinduzi CCM
Mbunge wa
viti maalumu mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati akizungumza jambo wakati wa kuwapokea wanachama hao wapya.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Chama cha mapinduzi (CCM)
manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimalisha kwa kuvuna wanachama watano kutoka
chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na
mikakati ya kuja kulikomboa jimbo la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama
cha CHADEMA.
Akizungumza wakati wa
kuwapokea wanachama hao kutoka kata ya kitwiru mwenyekiti wa CCM manispaa ya
Iringa Said Rubeya aliwapongeza wanachama kwa kutambua kazi inayofanywa na
chama cha mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano DR John Pombe
Magufuli.
“Mimi nimefurahi sana nyie
kurudi nyumbani maana mtakuwa na msaada mkubwa sana katika kukijenga chama hapa
manispaa ya Iringa ili tuweze kulikomboa jimbo hili katika uchaguzi ujao nah ii
ndio mikakati yetu”alisema Rubeya
Rubeya aliwaambia wanachama
hao kuwa sasa wapo katika mikono salama ya kisiasa tofauti na walipokuwa kwenye
chama cha awali na kuwasihi wasiwe waoga katika kufanya kazi za kukijenga chama
cha mapinduzi.
“CCm ni ndio chama tawala
hivyo ondeeni hofu na mzidi kutupa maarifa mliotoka nayo huko na kukisaidia
chama hiki kuzidi kupata wananchama wengi kutoka vyama vya upinzani na mkiwa
CCM mtapikwa vizuri na kuwa viongozi wazuri” alisema Rubeya
Aidha Rubeya aliwaambia kuwa
CCM hutoa madaraka kwa mtu yeyeto yule mwenye weredi katika nafasi aliogombe
hivyo huku hakuna kuteuana huku kuna nafasi za kugombea na kuchaguliwa na
wanachama cha mapinduzi tufati na kule mlikokuwa mnateuna kwa maslai ya mtu
mmoja.
Naye katibu wa chama cha
mapinduzi manispaa ya Iringa Marko Mbaga aliwataja wanachama waliohamia hamia
chama hicho kutoka CHADEMA ni Baraka Kimata aliyekuwa katibu mwenezi na Diwani
wa kata ya Kitwiru,Theodora Mbata aliyekuwa matroni wa wanawake kata ya Kitwiru,
Erick Muyungo na Raymond kimata
aliyekuwa kiongozi wa redbrigad manispaa ya Iringa na katibu mwenezi wa kata ya
kitwiru.
“Hii ni mwanzo tu watakuja
wengi mno kwa kuwa CCm manispaa ya Iringa wanachapa kazi hata kama halmashauri
ipo kwa wapinzania lakini wao wataendelea kufanya kazi kwa kutekeleza ilani ya
chama chetu ili kuwamaliza wapinzani wetu wote warudi kwenye chama tawala”
alisema Mbaga
Edwin bashir ni katibu wa
chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa alisema kuwa sasa ni wakati wa kufanya
kazi kwa wananchi na wananchi waendelee kuwa na Imani na chama cha mapinduzi
ili waje kufanikiwa kulikomboa hili jimbo ambao lipo upinzani.
“Mimi najua vijana wengi
muda sio mrefu wataanza kurudi nyumbani kwao kwenye chama wananchokipenda na
kuondokana na siasa za maji taka kwa kuwa CCM ni tanuli za kuwahoka viongozi
bora na sasa manispaa tutafanya kazi kweli kweli na kuwamaliza wapinzani kwa
nguvu zote” alisema Bashir
Baraka Kimata,Theodora Mbata,
Erick Muyungo na Raymond kimata walisema
kuwa watakitumikia ipasavyo chama cha mapinduzi kama walivyokuwa wanakitumika
chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na kuhakikisha CCM wanashinda chaguzi
zote watakazo kuwa wanashiriki katika manispaa ya iringa.
Kwa upande wake mbunge wa
viti maalumu mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati
aliwapongeza viongozi wote wapya waliochaguliwa hivi karibuni na kuanza kufanya
kazi inayoonekana machoni mwa wakazi wa manispaa hiyo.
“Juzi mmechaguliwa lakini
kazi imeanza kwa kuwapata wananchama wapya wanaotoka upinzani kurudi CCM hiyo
sio kazi ndogo kwa kweli hiyo ni kazi kubwa sana ambayo mmeanza nao nichukue
nafasi hii kuwapongeza kwa mnachokifanya kuhakikisha tunapata wanachama wengi
kutoka upinzani” alisema Kabati
0 comments:
Post a Comment