NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
TIMU
ya soka ya wafanyakazi wa Mwalimu Commercial Bank,(MCB), plc, imefungwa mabao
3-1 na kikosi mchanganyiko cha walimu wa jijini dar es salaam, katika pambano
la kirafiki ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya wiki moja ya walimu wa michezo
yaliyofanyika chuo kikuu cha dar es salaam.
Pambano
hilo lililopigwa kwenye uwanja wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, leo Oktoba 21,
2017, haikuwa kazi rahisi kwa kombaini ya walimu kushinda mchezo huo dhidi ya
“mabenker” hao wa MCB, kwani hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu zote
zilitoka sare ya bao 1-1.
Katika
kipindi cha pili tena dakika za lala salama, wafanyakazi wa MCB walielemewa na
kujikuta wanatundikwa mabao mawili ya haraka haraka.
Hata
hivyo kocha wa MCB, Lufingo Mwakilasa, aliwasifu wachezaji wake kuwa
wamejitahidi kucheza vizuri licha ya hali ya hewa kuwa mbaya (joto kali),
lakini pia asili ya kazi yao ambayo muda mwingi huwa wanautumia wakiwa
maofisini kuhudumia wateja ukilinganisha na wenzao ambao ni walimu wa michezo
na muda mwingi huwa wanafanya mazoezi.
Akizungumzia
pambano hilo la kirafiki, Mkuu wa
Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo, Valence Luteganya
alisema, kwa takriban wiki moja walimu hao wa michezo walikuwa wakishiriki
semina ya mafunzo chuo kikuu ambayo MCB ilidhamini semina hiyo.
“Mchezo huu ni wakujenga ushirikiano wa karibu na wenzetu walimu, ambao nao ni
wateja wetu wakubwa.”alisema Lutenganya.
Kombania ya walimu wa michezo wa jiji la Dar es Salaam, ambao walimenyana na wafanyakazi wa MCB katika pambano la soka la kirafiki. |
Priva Audax wa MCB, akijikunjua kufumua shuti.
Kocha mkuu wa MCB, Lufingo Mwakilasa
Wachezajiwa MCB (kulia), wakisalimiana na wwenzao wa Kombania ya walimu wa Dar es Salaam tayari kuanza mchezo huo.
Kipa wa MCB, akiruka kuokoa mpira
Kipa wa MCB, akipangua mpira
Priva Audax wa MCB
0 comments:
Post a Comment