Mwenyekiti wa chama cha waandishi Mkoani Geita,Daniel Limbe Akisisitiza Msimamo wa waandishi wa habari wakati wa kikao cha waandishi wa habari Mkoani Geita. |
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari Mkoani Humo wakati wa kikao cha maadhimio kwa Jeshi la Polisi. |
Baadhi ya waandishi wa Habari Mkoani Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya ofisi hizo. |
Na Joel Maduka.
Chama cha waandishi wa Habari Mkoani Geita Kimetangaza
Kutokushiriki kazi zozote za Jeshi la Polisi kutokana na fujo ambazo wamekuwa
wakifanyiwa waandishi wa habari wakati wakiwa kwenye majukumu yao ya kazi.
Uamuzi huo umefikiwa leo baada ya
kumalizika kikao cha dharula cha waandishi wa habari ambao walikutana
ili kujadiliana namna bora ya kukabiliana na unyanyasaji unaofanywa na
jeshi la polisi kwa waandishi wa habari mkoani Geita.
Tamko la kuondoa ushirikiano kwa jeshi
la polisi limesomwa na mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa
wa Geita Daniel Limbe (pichani),ambaye amesema uamuzi huo utatenguliwa
iwapo uongozi wa Jeshi la polisi mkoani humo utajitokeza kuomba radhi
kwa vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na polisi pamoja na
kuwahakikishia usalama wao wawapo kazini.
Aidha uamuzi huo umeanza kutekelezwa
baada ya tamko hilo huku ikielezwa kuwa mwandishi wa habari atakayekiuka
makubaliano hayo atachukuliwa hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kufutwa
uanachama wake ndani ya Klabu hiyo.
Uamuzi huo umekuja ikiwa ni siku mbili
zimepita tangu waandishi wa habari wanne kushambuliwa na kuharibiwa
vifaa vya kazi wakati wakichukua matukio ya vurugu zilizotokea kwenye
shule ya sekondari Geita(Geseco) ambayo pia wanafunzi walikuwa
wakitishia kuichoma moto iwapo wenzao watano waliokuwa wanashikiliwa na
jeshi la polisi hawataachiliwa huru na kulejea shuleni hapo.
Waandishi waliokutana na masaibu hayo na
vyombo vyao kwenye mabano ni Editor Edward(Mtanzania),Rehema
Matowo(Mwananchi),Ester Sumira(Azam Tv) na Emmanuel Ibrahimu(Clouds tv).
0 comments:
Post a Comment