Na Mathias Canal, Singida
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu
amezindua msimu wa kilimo 2017/18 ikiwa ni Sehemu ya kuwasihi wananchi
kuanza kujiandaa kwani tayari wakati wa kuanza kilimo umekaribia.
Katika
uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji na kata ya Ihanja wilayani
Ikungi Mhe Mtaturu pamoja na mambo mengine lakini amewasihi kutumia
vizuri mvua za mwanzo kupandia.
Katika
mkutano huo wa uzinduzi Mhe Mtaturu pia ameanzisha utaratibu huo wa
kuzindua msimu wa kilimo kila mwaka ili kuwaandaa wakulima kuingia msimu
mpya mapema ikiwemo kuyakumbusha makampuni ya mbegu kuwafikishia
wakulima mbegu kabla mvua kuanza kunyesha.
Sambamba
na utaratibu huo wa kuzindua msimu wa kilimo kila mwaka pia kutakuwa
na zoezi la kufanya maonesho ya zana na teknolojia mbalimbali za kilimo
ili wakulima wapate muda wa kujifunza mbinu mpya za kilimo ili kuongeza
uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Mhe
Mtaturu aliwaagiza maafisa ugani kuwa na mashaba darasa na madaftari ya
wakulima sambamba na kuwaunganisha wakulima hao na makampuni ya mbegu
ili waweze kupanda mbegu bora zikiwemo zile zinazokomaa kwa muda mfupi.
Aliwakumbusha
wakulima wote kulima mazao ya chakula ili kuwa na usalama wa chakula
ambapo aliyataja mazao hayo ambayo yanastahili hali ya ukame kuwa ni
pamoja na Mtama, uwele, Mpunga, viazi lishe,viazi vitamu na mihogo.
Pia
aliwataka wakulima kulima mazao ya biashara ili kuwa na uchumi imara
huku akitikisa msisitizo zaidi katika mazao ya kipaumbele katika wilaya
hiyo ambayo ni Korosho, Pamba na Alizeti.
Mhe Mtaturu aliwahakikishia wananchi kupanda mbegu mapema za korosho na dawa za kupulizia ili kuua vijijidudu vinavyoshambulia.
Alisma
kuwa tayari Wilaya ya Ikungi imepokea Mbegu Tani 20 za Pamba ambazo
zitaanza kusambazwa wiki ijayo kwa wakulima waliojiandikisha.
Akisoma
taarifa ya idara ya kilimo kwa Mkuu wa Wilaya, Kaimu afisa kilimo
Wilaya ya Ikungi Ndg Teendwa Senkoro alieleza lengo la wilaya hiyo ku
ni kulima hekta 124,038 za mazao mbalimbali katika msimu wa mwaka
2017/18 na kuvuna tani 208,700 za mazao mbalimbali.
Mhe
Mtaturu ametimiza ahadi yake ya kuanzisha msimu wa kilimo aliyoahidi
hivi karibuni wakati alipofanya kikao kazi na wakuu wa Idara na Vitengo
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Ally
Mwanga alimpongeza Mhe Mtaturu kwa juhudi zake mbalimbali za kimaendeleo
anazozifanya katika Wilaya hiyo tangu ateuliwe kuhudumu katika nafasi
hiyo.
Alisema
kuwa waheshimiwa Madiwani na Halmashauri wataendelea kumuunga mkono
katika jitihada hozo ili kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment