Mkurugenzi wa Viktoria Faundation Vicky Kamata akielezea madhumuni ya taasisi hiyo kutoa msaada wa kadi za matibabu. |
Moja kati ya wakina mama ambao ni wajane akifurahia baada ya kupatiwa kadi ya matibabu. |
afisa matekelezo wa mfuko wa bima ya afya Mkoani Geita,Paul Bulolo akitoa elimu ya matumizi ya kadi ya bima ya afya wakati wa shughuli ya kuwakabidhi wakina mama wajane mia moja. |
|
NA JOEL MADUKA.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Victoria
Foundation imetoa msaada wa kadi za bima ya afya kwa wakina mama wajane mia
moja(100)Mkoani Geita.
Akikabidhi Kadi hizo mapema leo
Mkurugenzi wa taasisi hiyo ambaye pia ni mbunge wa viti
maalum Mkoani humo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Vicky Kamata
alisema kuwa wameonelea ni vyema wakatoa msaada wa bima za afya kwa
wakina mama wajane kutokana na adha ambazo wamekuwa wakikutana nazo na
kwamba kundi hilo limesahaulika sana na wengi wao wanakuwa hawana uwezo
wa kujikimu gharama za matibabu pindi wanapokuwa wameugua.
“Wakina mama wajane tumeamua kuwasaidia
bima za afya kutokana na wengi wao wamekuwa awana uwezo wa kufanya shughuli
ambazo zinaweza kuwasaidia kiuchumi na wengine unakuta hata gharama za matibabu
kwao ni tatizo hivyo sisi tumeonelea kwa awamu hii ya kwanza tuanze na wakina
mama mia moja kasha tutaendelea na awamu nyingine tena”Alisema Kamata.
Pia ameongezea kuwa jumla ya kiasi cha
fedha ambacho kimetumika kugharamia kadi hizo za bima ya afya ni Milioni saba
na laki sita.
Kwa upande wake afisa matekelezo wa
mfuko wa bima ya afya Mkoani Geita,Paul Bulolo alisema pamoja na kutoa kadi
hizo kwa wakina mama lakini pia wamewaomba kutengeneza vikundi vya ujasiriamali
ambavyo vitawasaidia kujikwamua kiuchumi hali ambayo itawasaidia kuhuisha kwa
mala nyingine kadi za bima ambazo wamepatiwa siku ya leo.
“Kadi hii ya bima ya afya itakusaidia
kutibiwa sehemu yoyote na maeneo yoyote hapa nchini na hivyo basi tunajua kuwa
kadi hizi zinamwaka mmoja nilikuwa nawaomba wakinamama kutumia fursa hii kuunda
vikundi vya ujasirimali ambavyo vitawasaidia kuhuisha kadi zenu pindi
zinapokuwa zimemaliza muda wake”Alisisitiza Bulolo.
Bi,Maneshu Lema ni moja kati ya
wakinamama ambao wamenufaika na kupatiwa kadi ya bima ya afya pamoja na
kushukuru taasisi hiyo alisema kuwa miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakikutana
na changamoto ni pamoja na wajane na kwasasa wamesaidiwa kwa kiasi
kikubwa kwani hawatakuwa na mawazo ya gharama za kutibiwa .
0 comments:
Post a Comment