Shamba la Pamba. |
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Samweli Abuye akizungumza na wakulima wa Kijiji na Kata ya Kagu. |
Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa umakini maelekezo ya Kilimo cha pamba ambacho kinatarajia kuanza hivi karibuni. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na watendaji wa kata na vijiji na kutoa msisitizo wa kuwasisitiza wananchi kwenye maeneo yao kulima zao la Pamba. |
PICHA NA JOEL MADUKA
Wakulima wa zao la pamba katika tarafa ya Bugando
Wilaya na Mkoani ya Geita wamesema wamekuwa wakikata tamaa kuendelea na kilimo
cha zao hilo kutokana na sababu mbalimbali wanazokumbana nazo likiwemo suala la
pembejeo pamoja na bei za pamba kutokueleweka.
Wakizungumza katika kikao cha
maelekezo kwa watendaji wa serikali ya Vijiji na Kata kwenye ukanda wa tarafa
ya Bugando, wakulima wa zao hilo Faustin
Nyamhanga, Faida Mwendesha na Mateso
Kabegelo, wameyatupia lawama makapuni yanayojihusisha na ununuzi wa zao
hilo kwa kile walichodai kwamba wanakuja
na bei yao mkononi ambayo ni ya ughalalizaji.
Pamoja na mambo mengine, wameendelea kuikumbusha serikali kuendelea kuyapatia
ufumbuzi masuala ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kwa wakulima.
Diwani wa kata ya Nyamboge, Daudi
Bakazahala ameiomba Idara ya Kilimo Wilayani humo kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa
wa Geita ili kushughulika na wahasibu wa makampuni ya ununuzi wa pamba kwenye
maeneo ya vijijini ambao wamekuwa na tabia ya kuwaibia wakulima.
Kutokana na kero ambazo
zimeelezwa na wakulima pamoja Diwani, Mkaguzi wa Zao la pamba Wilaya ya Geita
Venance Kankutebe, amesema kutokana na uchache wa viwanda imekuwa ni changamoto
kwa upande wa bei, huku Afisa Kilimo Samweli Abuye akijibu ombi la diwani wa
Nyamboge kwa kubainisha kwamba ni vyema wao kama viongozi wa kata kumfikishia
mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Juu ya madai ambayo wamekuwa nayo
kwani yeye ndiye msimamizi mkuu wa kikosi kazi cha ufuatiliaji wa kilimo cha
pamba.
0 comments:
Post a Comment