Mabomba ambayo yanatoka kwenye mradi wa Nchakolongo yakiwa yametandazwa wakati Mkuu wa Wilaya ya Geita alipokwenda kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi pamoja na wataalam. |
Chanzo cha maji ambacho ndio kinatumika na wanakijiji wa kijiji cha Chikobe. |
Maduka Online .
Wakazi wa
Kijiji cha Chikobe Kata ya Nyachiluluma wilayani Geita wanakabiliwa na tatizo
la maji hali inayohatarisha afya zao kwa kutumia maji yasiyo safi wala salama.
Wakizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara baadhi ya
wananchi hao Bi Pili Simon Goi na Maganga Paul Walisema kuwa wamekuwa wakitumia
muda mrefu kutafuta maji na kwamba kumekuwa na mabomba yanayowekwa bila kutoa
maji huku kukiwa na mradi wa maji ulioanza mwaka (2010 )lakini haujakamilika
hadi sasa.
“Sisi wakina
mama ndio wahanga wakubwa ukosekanaji wa
maji kwani tumekuwa tukiamka usiku wa manane kwenda kutafuta maji na muda
mwingine tunakuwa na hofu kubwa kutokana na kuogopa kufanyiwa vitendo vya
ukatili likiwemo swala la kubakwa kwakweli tunatesekan Sana”Alisema Bi,Pili
Goi.
“Kuna mradi
ambao umeanzishwa tangu mwaka 2010 lakini jambo la kusikitisha hadi sasa mradi
huo ujakamilika na tunapata shida ya maji tunaomba serikali itusaidie juu ya
swala hili”Alisema Maganga Paul.
Akizungumza
kwenye Mkutano huo wa hadhara Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi
aliwataka wakazi wa kijiji hicho kuwa wavumilivu kwa kuwa tatizo hilo
litapatiwa ufumbuzi muda mfupi ujao.
Kaimu
mhandisi wa maji wa Wilaya ya Geita Bw Yusuf
Chalamanda alisema mradi wa maji wa Nchankolongo umechukua muda mrefu
kutokana na tatizo la fedha na baadhi ya wakandarasi kutokuwa waaminifu na
kwamba wanatarajia kuanza kufanya majaribio kwa kusambaza maji kwenye vijiji
vya Chikobe, Nchankolongo, Chiguga na Kabayozo na pia mradi huo utakamilika na kuanza kusambaza maji rasmi
Desemba 12 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment