Binagi Media Group
Mkuu wa
wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Nurdin Babu amewataka wananchi na watendaji wa
serikali, kuhakikisha wanashiriki na kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya
maji ili kutatua kero ya maji wilayani humo.
Babu ametoa
kauli hiyo hii leo wakati akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano ya
utekelezaji wa mradi wa kutatua kero ya maji wilayani Serengeti, baina ya
shirika la Amref Tanzania na halmashauri ya wilaya hiyo.
Mradi huo ujulikanao
kama “Rain Tanzania” unatekelezwa wilayani humo kwa kipindi cha miaka miwili kupitia
ufadhiri wa taasisi ya Cocacola Afrika katika Kata za Mosongo, Kenyamonta,
Busawe pamoja na Nyansurura, ukilenga kusaidia upatikanaji wa majisafi na salama
karibu na makazi ya wananchi ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu dolla za
Marekani sita.
Meneja wa mradi
huo, Mhandisi Japhet Temu amesema pia utasaidia kuhamasisha usafi wa mazingira,
ujengaji na utumiaji wa vyoo bora pamoja na kuwawezesha kiuchumi vijana na
akina mama ambapo vikundi 50 vya vijana na 20 vya akina mama vitawezeshwa
mafunzo na mitaji ya ujasiriamali.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa Amref Tanzania, Mturi James amewahimiza wananchi
kushiriki vyema kwenye utekelezaji na utunzaji wa miundombinu ya mradi huo ili
kuhakikisha unakuwa endelevu.
“Ndoa nyingi
zinapata shida pale ambapo wanawake wanakwenda kuchota maji umbali mrefu na
kuchelewa kurudi nyumbani”. Anasema Bi.Bwiru Elisha, mkazi wa Kijiji cha
Gantamome wilayani Serengeti.
Wilaya ya
Serengeti inakabiliwa na kero ya upatikanaji wa maji ambapo Mkurugenzi wa halmashauri
ya wilaya hiyo, Mhandisi Juma Hamis anasema kati ya miradi 10 ya maji katika
halmashauri hiyo, ni miradi miwili pekee imekamilika na kutoa huduma ya maji
kwa wananchi.
Mhandisi wa
maji katika halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Dickson Protas anasema wastani
wa matumizi ya maji kwa kila mwananchi ni lita tano kwa siku ingawa uhitaji ni wastani
wa lita 30 katika maeneo ya vijijini na lita 65 hadi 70 katika maeneo mjini.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kuanza utekelezaji wa mradi huo. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa halmashauri ya Serengeti, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mkazi Amref Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kuanza utekelezaji wa mradi huo. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa halmashauri ya Serengeti, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mkazi Amref Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Nurdin Babu akizungumza kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Juma Porini akizungumza kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Juma Hamsini akizungumza kwenye hafla hiyo
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa shirika la Amref nchini Tanzania, Mturi James akizungumza kwenye hafla hiyo
Katibu Tawala wa wilaya ya Serengeti, Cosmas Qamara, akizungumza kwenye hafla hiyo
Meneja mradi wa kutatua kero ya maji (Rain Tanzania) katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Mhandisi Temu Japhet akizungumza kwenye hafla hiyo
Godfrey Matumu ambaye ni Meneja mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti akizungumza kwenye hafla hiyo
Japhet Kisusi ambaye ni mwakilishi wa taasisi ya Cocacola Afrika, wafadhiri wa mradhi huo akizungumza kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Mhandisi Juma Hamis akisaini makubaliano ya mradi huo. Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa shirika la Amref nchini Tanzania, Mturi James na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Mhandisi Juma Hamis akisaini makubaliano ya mradi huo. Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa shirika la Amref nchini Tanzania, Mturi James
Baada ya makubaliano ya utekelezaji wa mradi huo kusainiwa
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo
Washiriki wa hafla hiyo
Washiriki wa hafla hiyo
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na washiriki wa hafla hiyo
Mashine za kuendesha miradi ya maji zitakuwa zikitumia nishati ya jua
0 comments:
Post a Comment