Na: Calvin Edward Gwabara
Morogoro.
Mtandao wa Elimu (TEN/MET) kwa kushirikiana na Action Aid Tanzania wawakutanisha walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania ili kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto zinazorudisha nyuma au kukwamisha jitihada zao za kutoa elimu bora nchini.
Meneja Miradi wa Mtandao huo, Mwalimu Alistidia Kamugisha (wa kwanza kulia) Akizungumza na waandishi wa habari juu ya Kongamano hilo. |
Akizungumza wakati wa utambulisho na lengo la kongamano hilo maalumu katika siku ya Mwalimu duniani, Afisa miradi ya mtandao huo Mwl. Alestidia Kamgisha alisema walimu wanachangamoto nyingi ambazo zisipotatuliwa zitaendelea kushusha ubora wa elimu kutokana na kuporomoka kwa hali ya mwalimu kufundisha.
“kukutana kwao kwa pamoja kutasaidia kila mmoja kusikia changamoto na mafanikio ya mwalimu mwenzake kutoka mkoa mwingine lakini pia kujifunza kwa walimu wengine waliofanikiwa wakiwa ndani ya changamoto hizo”, alisema Kamugisha.
Pia Afisa Miradi huyo wa mtandao wa elimu Tanzania aliongeza kuwa mawazo ya pamoja kutoka kwa wadau hao yatasaidia katika kubuni mbinu za pamoja kama wadau ili kusaidia kutatua chaangamoto hizo na kurudisha nguvu ya mwalimu katika kufundisha na kufaulisha.
Aidha akieleza hali ya shule yake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyandira mwalimu Atulinda Musebura alisema kuwa shule yake inawalimu watano tu lakini inazaidi ya wanafunzi 1000 idadi ambayo ni kubwa sana kwenye uwiano kati ya mwalimu mmoja na mwanafunzi.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyandira mwalimu Atulinda Musebura. |
“hali hii inatulazimu kufundisha kwakuelekeza nguvu kwa darasa la saba ili kuwawezesha wanafunzi hao kufaulu mitihani yao ya mwisho na wanapoondoka nguvu zetu tunazielekeza kwa darasa la nne ambao nao wanakuwa na mtihani wa Taifa,
Hali hiyo inawanyima wanafunzi wengine kwenye nyakati Fulani kukosa masomo na hata kuwatesa walimu hao kwa kufanya kazi kupita uwezo wao na mwalimu anapopata dharura hali huwa mbaya zaidi kwani walimu hao kila mmoja anavipindi zaidi ya 67 kwa wiki badala ya 40”,alisema Musebura.
Kwa upande wake muwezeshaji kwenye kongamano hilo bwana Zelote Loilang’akaki alisema mkakati wa serikali kutoa elimu bure umesaidia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wanafunzi mashuleni lakini swala la ongezeko la walimu halikuzingatiwa hivyo kuwafanya walimu kuzidiwa na mzigo wa kazi ya ufundishaji.
Muwezeshaji wa kongamano hilo Bwana Zelote Loilang’akaki akizungumza na washirki hao |
“Changamoto ya upungufu wa walimu umekuwa mkubwa kwa shule za msingi wakati wa idadi ya walimu wa Sayansi ikibaki kuwa ndogo kwenye shule za secondary kwamfano kuna upungufu wa walimu wa Sayansi 64 sekondari wakati msingi kunaupungufu wa walimu 614 kwa mujibu wa ripoti za TEN/MENT kwa wilaya ya Mvomero pekee”, alisema Loilang’akaki.
Pia alibainisha kuwa kwa mujibu wa serikali idadi ya walimu imeongezeka kufika 165,856 mwaka 2010 hadi 2011 hadi kufika 190,957 mwaka 2014 hadi 2015.
Taarifa za chama cha walimu Tanzania (CWT) zinaonyesha nchi inaupungufu wa walimu 100,000 kwa shule za msingi 500,000 shule za sekondari ambapo walimu wa Sayansi 30,000 na sanaa 20,000 huku taarifa za elimu ya msingi (BEST 2016) zinaonyesha upungufu ni walimu 7291 wa hesabu 5118 Biology 5375 kemia 6873 walimu wa fizikia.
Bwana Prosper Lubuva Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo (CWT) akiwasilisha mada juu ya mapendekezo ya Shirika la kazi duniani na ILO na UNESCO kuhusu hali ya walimu ya mwaka 1966. |
Mwalimu akiwa amefungwa kitambaa na kuagizwa kitu ukumbinu hapo ikiwa ishara ya kuona changamoto na vikwazo anavyokutana navyo Mwalimu kwenye kufikia malengo yake ya kufundisha na kufaulisha. |
0 comments:
Post a Comment