Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akizungumza wakati wa hafla ya kuwapokea madaktari kutoka jamhuri ya watu wa China ambao wataka Mafinga kwa takribani siku mbili kutoa huduma kwa wagonjwa mbalimbali na katikati yake ni mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William na waziri wa mambo ya nje dr Agustino Mahiga
Waziri wa mambo ya nje dr Agustino Mahiga akizungumza wakati wa hafla ya kuwapokea madaktari kutoka jamhuri ya watu wa China ambao wataka Mafinga kwa takribani siku mbili kutoa huduma kwa wagonjwa mbalimbali na katikati yake ni mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William na Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi
Picha ya pamoja ya viongozi wa Tanzania na madaktari kutoka katika nchi ya Jamhuri ya watu wa China
Baadhi ya wananchi waliofika katika hafla ya kuwapokea madaktari hao tisa kutoka katika nchi ya Jamhuri ya watu wa China.
Na Fredy Mgunda,Mafinga.
Jumla ya madaktari tisa
kutoka jamhuri ya watu wa china wapo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa
ajili ya kusaidia kuwatimu wangonjwa wenye magonjwa sugu na magonjwa yasiyo
sugu lakini madaktari hao wamepatikana kwa ushirikiano wa mbunge wa jimbo la
Mafinga Mjini Cosato Chumi na waziri wa mambo ya nje dr Agustino Mahiga.
Akizungumza na blog hii
mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi alisema kuwa lengo na kuja kwa
madaktari hao ni kubadirishana uwezo na ujuzi kwa madaktari wazawa ili
kuendelea kuboresha sekta ya afya kwa wananchi wa jimbo hilo na wana wanaokuja
kupata huduma katika hospitali za Mafinga.
“Hospitali ya Mafinga
imekuwa ikihudumia wananchi kutoka halmashauri mbalimbali na mikoa mbalimbali
kutokana na jeografia yake ilivyo,hii hospitali ipo katika barabara kuu hivyo
wananchi wote wakipata shida ya ugonjwa wowote wanakimbilia hapa hivyo ni
lazima tuboreshe sekta ya afya ili kuokoa maisha ya wananchi wetu” alisema
Chumi
Chumi ameongeza kuwa madaktari
hao watakuwa wakitibu magonjwa yote mfano macho,mifupa,uzazi koo na kadharika
hiyo ni faida kubwa kwa wananchi na madaktari wazawa kujifunza au kupata elimu
kutoka wa madaktari kutoka nchi ya China.
“Sio kuwa madaktari wetu
hawana uwezo ila kujengeana uwezo au kujifunza ni jambo la kawaida hasa katika sekta
kama hii ambayo inaumuhimu sana katika maisha ya mwanadamu”alisema Chumi
Naye waziri wa mambo ya nje
dr Agustino Mahiga aliwataka viongozi
kutoa ushirikiano wa kutosha kwa madaktari hao kwa kuwa wao ndio wenyeji na
wanajua mambo mengiya hapa Tanzania hapa wilaya ya Mufindi kuliko hao
madaktari.
“Kiukweli sisi watanzania
tunajijua tabia zetu hivyo naomba tufanye yaliyo mema na kuonyesha ushirikiano
wa kutosha kutoka kwa hawa madaktari ambao najua tutajifunza kitu kutoka kwao”
alisema Mahiga
DR Mahiga alisema kuwa Tanzania
na China zimekuwa na ushirikiano mzuri hivyo yatupasa kuendelea kudumisha
ushirikiano huu ambao unafaida kwa nchi zote mbili.
Naye mkuu wa wilaya ya
Mufindi Jamhuri Wiliamu aliwakikishia viongozi hao kuwa madaktari hao kutoka
jamhuri ya watu wa China watapewa ushikiano mzuri ili wakiondoka wakatoe sifa
nzuri huko kwao.
0 comments:
Post a Comment