Mwenyekiti chama
cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
mkuu wa wilaya ya
Mufindi Jamhuri Williamuakizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Na Fredy Mgunda,Mufindi
Chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya
ya Mufindi mkoani Iringa kimemuomba mkurugenzi kuwakopesha viwanja walimu ili
kujikwamuamua na mazingira magumu wanayokumbana katika nyumba wanazoishi.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti chama
cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale alisema kuwa walimu
wamekuwa wakiishi katika nyumba chakavu au mbali na mazingira ya shule kitu
kinachosababisha kushuka kwa uwezo wa walimu kufundisha.
Kimbale alisema kuwa walimu hawana
pesa za kununua moja kwa moja viwanja hivyo kwa njia ya kuwakopesha inawezekana
kutokana kuwa ni waajiliwa wa serikali na mishahara yao inajulikana na ni
rahisi kuresha mkopo huo.
“Sisi walimu ukitaka kujua mimi
nalipwa shilingi ngapi ni rahisi tu kwa kuwa mishahara ya serikali mara nyingi
inajulikana hasa pale mtumishi unapoenda kukopa mahali ndio maana tunaiomba
serikali itusaidie kukopa viwanja kuwa kuwa tunauwezo wa kulipa kwa awamu tatu”
alisema Kimbale
Aidha Kimbale aliwatupia lawama
maafisa elimu na walimu wakuu wa shule kwa kuwanyima ruhusa bila kuwa na sababu
maalum.
“Wakurugenzi amekuwa ametoa kibali
upewe ruhusa lakini viongozi waliochini ya mkurugenzi wanatuwekea vipingamizi
ambavyo havieleweki kitu kinachozua utata mkubwa baina ya viongozi na walimu
ambao sio viongozi” alisema Kimbale
Kimbale alimpongeza wakurugenzi wa
halmashauri ya mufindi na mji wa mafinga kwa kuwajali walimu kwa kuwapa ruhusa
pale inapotakiwa tofauti na hali ilivyo kwa hawa viongozi wa chini yake.
“Unakuta siku ya wanawake duniani au
siku ya walimu duniani bado walimu wananyimwa ruhusa wakati muda huo mkurugenzi
amewaruhusu walimu kuhudhuria sherehe hizo kitu kinachoongeza ukakasi baina ya
watendaji wa nafasi za juu na watendaji wa nafasi za chini” alisema Kimbale
Kimbale aliwapongeza walimu wa
manispaa ya Iringa kwa kuendelea kufanya kazi kwa kujituma licha ya kukumbana
na changamoto mbalimbali ikiwepo kunyimwa ruhusa.
Akijibu hoja hizo mkuu wa wilaya ya
Mufindi Jamhuri Williamu alisema haelewi kwanini mara kwa mara swala hilo
linakuwa linajirudia maana tulishalitafutia ufumbuzi hapo awali.
Sasa naenda kuandika barua rasmi kwa
wakurugenzi ili kutatua kabisa tatizo hilo maana hata kwangu imekuwa kero na
mwazoni nilijua wakuu wa shule ndio tatizo kumbe maafisa elimu ndio tatizo
naenda kulishughulikia kwa haraka sana swala hili” alisema Williamu
Williamu aliwataka maafisa elimu na
wakuu wa shule wote wa wilaya ya Iringa kuwapa ruhusa walimu pale ambapo
wanapata matatizo maana hakuna haja ya kumnyima ruhusa mtu akiwa anashida na
watakiwa kuzifahamu siku za kitaifa ambazo ni lazima walimu wahudhurie
wanapaswa kutoa ruhusa bila kipingamizi.
“Kunasiku kama siku ya mwalimu,siku
ya wanawake na siku nyingine za kitaifa walimu wanapaswa kupewa ruhusa kwenda
kuhudhuria tukio hilo kutokana na umuhimu wake” alisema Williamu
Williamu alisema kuwa mkurugenzi
ndio mwajili sasa hao maafisa elimu na wakuu wa shule wanatoa wapi hiyo jeuri
ya kuwanyima ruhusa ambayo viongozi wa ngazi za juu wanajua kuwa kunakitu
kinafanyika cha taifa.
Williamu aliwataka viongozi wa
walimu kuandika barua ya kuomba viwanja ili waweze kulishughulikia swala hilo
likiwa kwenye maandishi.
“Andikeni barua yenye idadi na
majina ya walimu wanaotaka viwanja ili kuondoa kasumba ya kusema wanaotaka ni
kikukindi cha walimu wachache tu na bila kufanya hivyo swala lenu la kuomba
viwanja litakuwa gumu kulitafutia ufumbuzi” alisema Williamu
Williamu aliwaomba walimu
wawewavumilivu katika kipindi wacholishughulikia swala hilo kwa kuwa sio jambo
la kukurupuka linahitaji utulivu wa kutosha ili kufanikishwa swala walimu
kupata viwanja.
Naye afisa elimu wa wilaya ya
Mufindi alisema kuwa watawatafuta hao maafisa ambao wanawanyima ruhusa walimu
wakati swala hilo lilishatafutiwa ufumbuzi.
“Jamani sisi huku sheria
tulishaiweka kwenye matukio muhimu ya kitaifa walimu wapewe ruhusa sasa sijui
ili sawala limetoka wapi naomba nikitoka hapa nitazungumza na wakuu wa shule
pamoja na maafisa elimu wenzangu”
0 comments:
Post a Comment