Mwenyekiti
chama
cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu
Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano mkuu wa chama hicho wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Na
Fredy Mgunda,Mufindi
Chama
cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimeitaka serikali ya
jamhuri ya muungano wa Tanzania kutatua changamoto za walimu ili kukuza na
kuboresha sekta ya elimu ambayo ndio kiungo muhimu katika maendeleo ya nchi
yoyote duniani.
Akizungumza
wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho mwenyekiti wilaya ya Mufindi Obi Kimbale
aliitaka serkali kulipa madeni wanayoidaiwa na walimu ili kuboresha maisha ya
walimu ambao wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu.
“Walimu
tunadai madeni ya malimbikikizi ya mishahara,madaraja tatizo kubwa na walimu
wanadai madeni ya likizo hivyo walimu wanakuwa hawana morali ya kufndisha
kutokana na kutolipwa stahiki zao kwa wakati” alisema Kimbale
Kimbale
alisema kuwa kutoka mwaka 2016 hadi hii leo walimu wa wilaya ya Mufindi
hawajalipwa stahiki zao hivyo kupunguza kasi ya walimu kuwa na wabunifu wakati
kuandaa maandalio ya kwenda kuwafundisha wanafunzi ili wapate elimu bora.
“Serikali
ililipa madeni kidogo sana miaka ya nyuma hivyo bado serikali tunaidai pesa
nyingi za walimu wa wilaya ya mufindi hivyo naitaka serikali kulipa madeni yote
wanayodaiwa na walimu ili kuwaacha walimu wafundishe wakiwa huru kwa kupata
stahiki zao zote” alisema Kimbale
Aidha
Kimbale aliwaomba walimu kuendelea kuwafundisha wanafunzi kwa moyo wao wote
wakati viongozi wao wanavyoshugulikia swala la madeni wanayoidai serikali.
Akijibu
hoja hizo mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William alikiri kuwepo kwa
changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu katika wilaya hiyo na kuahidi
kuanza kuzitafutia ufumbuzi.
“Kweli
kuna changamoto za miundombinu,stahikiza walimu na tatizo la upungufu wa walimu
serikali inayafanyia kazi hayo yote ili kumfanya mwalimu afanye kazi yake kwa
weledi unaotakiwa” alisema William
William
aliwataka walimu kudhibiti nidhamu ya walimu na wanafunzi ili kumaliza tatizo
utoro mashuleni ambao umekuwa ukisababisha wanafunzi wengi kushindwa kufaulu
masoma yao na wengine kupata mimba wakiwa na umri mdogo.
“Mufindi
kumekuwa na tatizo la wanafunzi wengi kupata mimba wakiwa na umri mdogo
kutokana na utoro hivyo nawataka walimu kudhibiti nidhamu mashuleni na
kupunguza hizi mimba za utotoni” alisema William
Aidha
William aliwataka walimu kuacha kufanya siasa mashuleni ili kuboresha elimu kwa
kizazi wanachokifundisha na kupata matunda mema hapo baadae.
0 comments:
Post a Comment