Watu
15 wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa
wakisafiria kupinduka eneo la Ntembwa ndani ya Hifadhi ya Lwafi
wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
Ajali
hiyo imetokea jana Jumanne saa mbili usiku baada ya lori aina ya Fuso
lililokuwa likitoka Kijiji cha Mvimwa kuelekea Kijiji cha Wampembe
kupinduka. Lori hilo lilikuwa limebeba mahindi na abiria.
Kutokana
na ajali hiyo, Rais John Magufuli amemtumia rambirambi Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa, Zelothe Stephen, familia za marehemu, ndugu, jamaa na marafiki
walioguswa na vifo hivyo.
Katika
taarifa ya Ikulu, Rais Magufuli amewaombea majeruhi wa ajali hii wapone
haraka ili warejee katika afya njema na kuungana na familia zao katika
maisha yao ya kila siku.
Rais
Magufuli amezitaka mamlaka zinazohusika na usalama barabarani kuongeza
juhudi zitakazowezesha kukabiliana na matukio ya ajali ili kuokoa maisha
ya watu na mali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando katika taarifa amesema lori hilo liligonga mwamba kabla ya kupinduka.
Kyando
amesema watu 12 walikufa papo hapo na wengine watatu walifariki baada
ya kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa. Amesema dereva wa lori
hilo alikimbia baada ya ajali kutokea.
0 comments:
Post a Comment