na oliver motto,iringa
Kukithiri
kwa biashara haramu ya ngono pamoja na tabia ya ushoga mkoani Iringa
kunadaiwa kusababishwa na baadhi ya vijana wa vyuo vikuu waonafika
mkoani humo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu, huku miongoni mwao
wakitaka starehe zilizo nje ya uwezo wao.
Tamaa
ya kumiliki vitu vya thamani – ni miongoni mwa mambo yanayotajwa
kuwahadaa baadhi ya wasomi hao wa vyuo vikuu, jambo linalosababisha
wengi wao kuangukia katika wimbi la biashara ya ngono na ushoga na
kuufanya ongezeko la maambukzi ya vvu.
Kwa
mkoa wa iringa inadaiwa kuwa zaidi ya mashoga 1500 wamejitangaza
wenyewe kuendesha biashara haramu ya ngono, jambo ambalo kiafya
linadaiwa kuwa ni hatari kwa maambukizi ya virus vya ukimwi.
Baadhi
ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa ndiyo wanaonyooshewa kidole
kuhusika na biashara hiyo ya ngono na tabia ya ushoga- ambapo shirika la
restless development linalojihusisha na masuala ya afya ya uzazi na
makuzi kwa vijana- kupitia mradi wa dance for life- limewakutanisha
viongozi hawa wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa- ili
kujadili namna ya kujinasua katika wimbi hilo la ushoga na biashara
haramu ya ngono.
Serikali
inaona tatizo hilo la ushoga na biashara ya ngono litamalizwa na jamii
yenyewe, endapo tu wazazi na walezi watakemea mapema mienendo
hatarishi ya vijana wao.
Ushoga
ni tabia inayofanywa na baadhi ya wanaume, kwa kujihusisha kimapenzi
na wanaume wenzao, suala ambalo kwa kiwango kikubwa linatajwa
kuchochewa na mambo ya utandawazi, ambao unaibua mitindo mbalimbali na
tabia mpya kila uchwao.
0 comments:
Post a Comment