Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT), Mkoa wa Iringa, Zainab Mwamwindi
UMOJA wa Wanawake
wa chama cha mapinduzi UWT mkoa wa Iringa, umeuomba uongozi wa rais wa
awamu ya tano dk. John Magufuli- kuendeleza mapambano, kwa kuibua yale yote
yaliyofichika, zoezi linalofahamika kama ‘Utumbuaji wa majipu” kwa madai
kuwa nao UWT wanaziunga mkono jitihada hizo zinazoendele.
Hayo
yamezungumzwa na Zainabu Mwamwindi mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa chama cha
mapinduzi UWT Mkoa wa Iringa, wakati akinamama wa umoja huo – wakikabidhi
misaada mbalimbali ya kijamii kwa wagonjwa wa Kituo cha afya cha Idodi.
Bi -
Mwamwindi amesema mpango wa “Utumbuaji majipu” licha kuwa na tija kwa wananchi,
pia unakinaimarika chama cha mapinduzi -tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla
ya uongozi wa Dr.John Magufuli.
Rose Tweve
mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa, anasema Mpango wa utumbuaji Majipu
umelenga kuinua hali ya uchumi na kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu na
afya, huku Mwajemi Balagama katibu wa UWT mkoa wa Iringa akisema
jambo hilo la Utumbuaji Majipu ni jema na linapaswa kuungwa mkono na kila
mwenye utashi- huku akiwasisitiza wananchi juu ya suala la uimarishaji wa afya.
Akinamama
hao wa UWT mkoa wa Iringa wametoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa
katika kituo cha afya cha Idodi -zikiwemo Sabuni, Mafuta, Miswaki, dawa za
kusuguklia meno nk, misaada iliyoambatana na shughuli ya usafi, kwa kufagia
mazingira ya kituo hicho cha afya cha Idodi –zoezi lililoambatana na upandaji
wa miti katika shamba la UWT lililopo Tungamalenga.
0 comments:
Post a Comment