Leo Waziri wa Mambo ya ndani Charles Kitwanga leo amekutana na waandishi wa habari Dar es salaam.
Baada
ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya ofisi za Jeshi la Polisi
kikubwa alichozungumza ni kuhusu ugaidi, ubambikaji kesi kwa wananchi,
matumizi ya TEHAMA pamoja na madawa ya kulevya.
Mikakati ya kupambana na dawa za kulevya hapa nchini..“Nimepata
maelezo ya kutosha kuhusu kinachoendelea…kitakachotusaidia ni lazima
tuwe na mfumo mzuri wa kuhakikisha madawa ya kulevya hayaingii katika
nchi yetu, kwangu orodha ya wahusika hainisadii, kinachosaidia ni
kuhakikisha madawa hayaingii na yale yaliyopo yanatafutwa na kukamatwa
na wahusika wanafikishwa katika vyombo husika”..Charles Kitwanga.
“Tumekubaliana
Tutaanza utekelezaji wa mara moja, kuhakikisha tunaongeza nguvu
kuhakikisha mfumo mzima wa usambazaji na uingizaji tunauvunja”.
Askari Polisi kukosekana katika bandari ya Dar es salaam...”Tumelijadili
na tutajadiliana na wenzetu tuone ni utaratibu gani utatuwezesha
kuhakikisha bandari yetu inakuwa salama, kama kuna askari amekosea
anachukuliwa hatua na si kuvunja mfumo mzima”…
Ubambikaji kesi wananchi..“Tumelijadili
na wenzangu Polisi wamejipanga vizuri kuhakikisha kwamba kabla ya
mashtaka tuhakikishe kwamba mtu aliyekamatwa ashtakiwe kwa kosa
alilolifanya na si kupewa makosa ya kufikirika” na hili tutashirikiana
na wenzetu wa sheria na katiba”.. .
Msongamano wa magari Dar es salaam na kwingineko..“Tutaboresha zaidi ili kuhakikisha haya malalamiko ya wanannchi yanakuwa hayapo”.
Matumizi ya TEHAMA...”Matumizi
ya teknolojia ndani ya jeshi ikiwemo CCTV, matumizi ya kusajili magari,
leseni, ulipaji faini kwa kutumia tehama..Haya tumeyajadili na yote
yatafanyiwa kazi kwa wakati mmoja kisha kutolewa ufafanuzi…Charles
Kitwanga
Idadi ya askari waliopo na mikakati ya kuwapati makazi...”Tuna
idadi ya askari 45,000 ambao bado hawatoshi, wanaokaa katika nyumba za
Polisi ni kama 10,000 tu, tuna upungufu wa nyumba kama 35,000, tuna
mpango wa kujenga nyumba nyingine kama 5,000, tutajenga polepole
kuligana na uwezo wetu, nia ni kuhakikisha a skari wote wanakaa sehemu
moja ili kurahisisha ufanyaji kazi”..
0 comments:
Post a Comment