ABIRIA
zaidi ya 1000 waliyokuwa wakisafiri na treni ya Kampuni ya Reli
Tanzania (TRL), jana wamekwama mkoani Dodoma na kushindwa kuendelea na
safari kutokana kuanguka treni ya mizigo kati ya Kituo cha Itigi na
Kitakaa.
Tukio
la kukwama abiria hao limetokea juzi saa 2:00 asubuhi mjini hapa mara
baada treni hiyo ya abiria ilivyo kuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea
Tabora, Kigoma na Mwanza kuzuiwa na Mkuu wa Kituo cha Dodoma.
Akizungumza
jana asubuhi na wandishi wa habari mjini hapa Mkuu wa Kituo hicho cha
Dodoma, Suzo Kazimoto, alisema uongozi wa TRL umemalizika kuzuia
kuendelea kwa safari ya abiria hao kutokana kuelezwa mapema kuwa huko
waliko kuwa wakielekea kumetokea ajali.
Alisema
baada ya kupata taarifa ya kuanguka treni hiyo waliona ni vema kuzuia
katika kituo hicho kwa vile abiria hao wangeweza kupata huduma zote za
kijamii zinazohitajika baadala ya kuiruhusu kwani huenda wangeenda
kwamba katika eneo ambalo halina huduma hizo muhimu.
“Taarifa
tulizonazo ni kwamba mafundi wako kwenye eneo wanaendelea na kazi ya
kurejesha na tumewatangazia abiria wetu kuwa safari yao itaendelea
kuanzia saa 12:00 jioni leo(Jana),” alisema Kazimoto.
Akizungumzia
malalamiko ya abiria kwamba baadhi yao walikuwa hawana fedha za
kujikimu, Kazimoto, alisema wakati huo walikuwa wakikusanya idadi halali
ya abiria wenye tiketi ili aweze kufanya mawasiliano na Makao Makuu Dar
es Salaam kwa ajili ya kupata kibali cha kuwapatia abiria hao fedha ya
kujikimu.
“Hata
kama leo, ni nusu siku kwamba benki zinafungwa mapema hilo siyo tatizo
tutaangalia kilichopo ili tuweze kuwa saidia abiria wetu,” alisema
Kazimoto.
Awali
baadhi ya abiria walilalamikia uongozi wa Shirika hilo kushindwa
kujenga njia mbili tangu walipokabidhiwa reli hiyo na mkoloni kwani kama
kungekuwa na njia mbili kama ilivyo katika nchi nyingine safari yao
ingeendelea bila mvutano kama huo.
Mmoja
wa abiria hao, Khadija Salum ambaye alikuwa akielekea Kigoma huku akiwa
na mtoto mdogo alikuwa akilia njaa baada ya kuibiwa Sh. 70,000 ambazo
zilikuwa ni kwa ajili ya kujikimu wakati wa safari hiyo.
Pia,
alisema kuwa baada ya kukwama katika kituo hicho baadhi ya wafanya
biashara walipandisha bei za bidhaa ghafla hivyo kuwaongezea ugumu
katika kumudu kununua bidhaa hizo ikiwemo maji ya kunywa na chakula.
0 comments:
Post a Comment