Mtu mmoja
aliyejulikana kwa jina la Jophrey Mhongole (37) amekutwa ameuawa kwa kuchomwa
na kitu chenye ncha kali na watu wasiofahamika kisha mwili wake kuwekwa chini
nyuma ya gari lake lenye namba za usajili T850ACC aina ya Toyota mark II.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema mauaji hayo yalitokea Novemba 28, mwaka
huu saa (kumi na moja)11.00 alfajiri eneo la TRM-minyarani kihesa, manispaa ya
Iringa.
Kamanda Mungi alisema
kuwa baada ya polisi kupata taarifa walikwenda eneo lilipotokea mauaji hayo
ambapo walipofanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa Jophrey Mhongole aliauawa
kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiofahamika na kumweka chini
nyuma ya gari lake baada ya kumkuta na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha
kali sehemu za mwili wake.
Alisema haikuweza
kufahamika mauaji hayo yalilenga nini kwani Mhongole alipopekuliwa na polisi
alikutwa na fedha kiasi kikubwa(hakutaja kiwango alichokutwa nacho), simu yake
ya mkononi pamoja na gari lake.
Alisema kuwa polisi
inaendelea kuwatafuata waliofanya mauaji hayo, kufanya uchunguzi wa tukio hilo
ikiwa ni pamoja na kufahamu chanzo mauaji hayo na kuwa wakikamatwa watafikishwa
mahakamani.
Katika tukio lingine
mtembea kwa miguu amefariki dunia wakati akipata matibabu katika hospitali ya
Rufaaya Iringa baada ya kugongwa na pikipiki isiyofahamika namba wala mtu
katika eneo la mnazi mmoja,Kitwiru manispaa ya Iringa barabara ya Iringa/Mbeya.
Kamanda Mungi alisema
mtembea kwa miguu aitwae Ektori Kipalile (55) mkazi wa Igangidungu, Iringa
Vijijini aligogwa na pikipiki isiyofahamika namba wala mtu Nov.29 saa 3.00
usiku na kufariki wakati akipata matibabu.
Kamanda Mungi alisema
chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mwendesha pikipiki huyo ambaye hakujali
matumizi ya barabara kwa watembea kwa miguu.
0 comments:
Post a Comment