WAZIRI
wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya Ndani,
Charles Kitwanga, wameunda kamati ndogo ya wataalamu kwa ajili ya
kutatua changamoto zilizopo magerezani.
Wakizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara katika magereza
yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam, mawaziri hao wakifuatana na
makatibu wakuu wao, walisema wameshuhudia shangamoto kadhaa ambazo
wameamua kuziundia kamati kwa lengo la kuzitatua.
“Leo
tumezunguka katika magereza na tumeshuhudia changamoto kadhaa ambazo
tunaunda kamati ndogo ya wataalamu, kutatua changamoto hizo na Januari
tutarudi tena huku tukiwa na baadhi ya majibu ya baadhi ya changamoto
hizo na kuwaeleza wapi tumefikia katika kutatua changamoto nyingine,”
amesema Dk Mwakyembe.
Dk
Mwakyembe alisema ana matumaini makubwa kwamba watafika mbali katika
matarajio ambayo Rais John Magufuli anatarajia kuifikisha nchi, ambapo
alitaja changamoto walizozishuhudia kuwa ni pamoja na msongamano wa
wafungwa na mahabusu magerezani, uhaba na uchakavu wa nyumba za askari
pamoja na ubovu wa miundombinu iliyopo magerezani na vitendea kazi.
“Serikali
hii ya Awamu ya Tano kama ambavyo mmeona, imeanza kwa kasi ya kuwaletea
matumaini makubwa wananchi, matumaini ambayo yanahitaji wizara zote
kutengeneza mazingira wezeshi kuleta mabadiliko makubwa,” alisema Dk
Mwakyembe.
Alisema
moja ya Wizara muhimu zinazotegemewa kutengeneza mazingira wezeshi ili
kupiga hatua ni wizara zao kwa sababu zina vyombo vinavyotoa huduma za
haki kwa wananchi katika kukamata, kufungua mashitaka, kuhukumu na
kuhifadhi watu gerezani.
Kutokana
na mambo hayo, ndiyo maana waliamua kufanya ziara ya pamoja kutembelea
mazingira ya magereza ya Segerea, Keko na Ukonga, kujifunza changamoto
zilizopo katika magereza hayo ili waweze kuunganisha nguvu kutatua
changamoto hizo.
Alisema
katika msongamano magerezani, wamejifunza magereza yamekuwa yakibeba
zaidi ya mara mbili ya uwezo wa magereza hayo na hiyo inatokana na
ucheleweshaji wa kesi, unaofanyika katika vyombo ambavyo viko chini ya
wizara hizo.
0 comments:
Post a Comment